Wednesday, July 29, 2015

FASTJET YAZINDUA RASMI ‘ROUTE’ YA DAR- LILONGWE KWA KISHINDO

IMG_9496
Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati, akizungumza na abiria kwanza kuingia ndani ya ndege, Bi.Fatma Amour (aliyeipa mgongo kamera) kabla ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua ‘route’ mpya ya Dar-Lilongwe.
……………………………
Na Andrew Chale, modewjiblog
(Lilongwe-Malawi) Shirika la ndege la Fastjet  limeendelea kupanua wigo wake  baada ya mapema Julai 27 kuzindua kwa kishindo ‘route’ yake mpya ya kutoka Dar es Salaam- Tanzania kwenda Lilongwe-Malawi ambapo kwa wiki itakuwa ikienda mara mbili, kati ya Jumatatu na Ijumaa.
Katika uzinduzi huo Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati aliweza kukata utepe kuashiria rasmi kuanza kwa safari ya Lilongwe Malawi huku abiria mbalimbali wakipata kusafiri kwa mara ya kwanza na ndege hiyo kubwa kuelekea Malawi.
Uwanja wa Kimataifa wa Kamuzubanda, Lilongwe Malawi, ndege ya fastjet iliweza kuwasili katika uwanja huo majira ya saa sita mchana na kupokelewa kwa shangwe na wenyeji wananchi wa Malawi wakiongozwa na maafisa wa Serikali akiwemo Waziri wa Usafirishaji na Ujenzi wa Malawi, Mh. Francis Kasaila, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo, Bw Wilbrod Kayombo  na wengine wengi ambao hawakusita kuonyesha furaha yao.
IMG_9510
Mhudumu wa ndege ya Fastjet, Omar Ramadhan akikagua tiketi ya abiria wa ‘route’ mpya ya Dar-Lilongwe iliyoanza safari zake jana jijini Dar es Salaam, ambapo wateja wa Fastjet watapata nafasi ya kusafiri na ndege hiyo itakayokuwa ikifanya safari zake mara mbili kwa wiki ambapo ni Jumatatu na Ijumaa.
Akitoa hutuba fupi ya tukio hilo la kihistoria, Waziri wa Usafirishaji na Ujenzi wan chi hiyo, Mh. Kasaila anasema  ujio wa fastjet nchini mwake utaongeza fursa za kiuchumi  kwa kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuitumia nafasi hiyo ya usafiri wa anga kukamilisha shughuli zao popote pale ndani ya nchi jirani, Afrika na duniani kote.
Naye Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo, Wilbrod Kayombo ametoa rai yake kwa mamlaka husika  za nchini Tanzania kuimarisha vitega uchumi na maeneo ya fursa za kibiashara ili kuondoa usumbufu kwa wateja wa nje ambao ndio wanategemea bidhaa hizo muhimu.
“Naomba mamlaka za jiji kuboresha maeneo ya kibiashara. Mfano mzuri Kariakoo wafanyabiashara wengi wanaotoka hapa Malawi na kwenda kununua bidhaa zao Kariakoo Dar es Salaam. Hivyo kama kuna matatizo mamlaka zinatakiwa kutatua haraka kwani wanaoteseka ni wageni wanaotoka mbali” anasema, Kaimu Balozi Kayombo.
IMG_9516
Abiria wakiendelea kuingia ndani ya ndege hiyo.
Kaimu Balozi Kayombo anasema Fastjet itakuwa mkombozi namba moja  nchini humo huku akitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wa Tanzania kuitembelea Malawi na kujionea fursa za ndani.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa fastjet kwa Afrika Mashariki, Jimmy Kibati anasema ni furaha kwao kuweza kusogeza huduma zaidi  kwa wateja waliokuwa wakitumia muda mrefu kusafiri kutumia usafiri mwingine kufika nchini humo… sasa wamepata mkombozi ambaye ni Fastjet na  kwa gharama nafuu kabisa huku akiomba waendelee kuwaunga mkono.
Kwa upande wake, Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro anasema awali Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘route’ za Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar na baadae kuweza kuvuka mipaka zaidi kwa nchi za Afrika kwa ‘rouet’ kati ya Dar – Johannesburg (Afrika Kusini), Dar – Lusaka (Zambia), Dar – Harare (Zimbabwe), Dar – Entebbe (Uganda) na kwa sasa hii ya Dar-Lilongwe (Malawi).
Afisa huyo, anaeleza kuwa, Fastjet itaendelea kutoa huduma bora kupitia usafiri wa anga huku akisisitiza kuwa ‘route’ mbalimbali zikiwa mbioni kufikiwa na shirika hilo.
IMG_9550
Mhudumu wa Shirika la ndege la Fastjet, Ernest Robert akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya usalama iwapo itatokea dharura ndani ya ndege kwa abiria kabla ya kuanza safari ya Dar-Lilongwe iliyozinduliwa jana.
IMG_9591
Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (katikati) akikata cake maalum ndani ya ndege safarini kuelekea Lilongwe kama shamra shamra ya kupamba uzinduzi wa ‘route’ hiyo mpya huku Wahudumu Grace Lukondo na Omar Ramadhani wakishuhudia tukio hilo.
IMG_9609
Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akikabidhi kipande cha cake kwa abiria wa kwanza kuingia ndani ya ndege hiyo Mjasiriamali Fatma Amour, aliyekuwa akielekea nchini Malawi kwa shughuli za kibiashara.
IMG_9650
Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kulia) akipeperusha bendera ya nchi ya Malawi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kamuzu jijini Lilongwe, Malawi. Kushoto, Bw. Jude Mkai kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
IMG_9676
Abiria wa ‘route’ mpya ya ndege ya Fastjet ya Dar-Lilongwe wakiteremka kwenye ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu, jijini Lilongwe.
IMG_9690
Waziri wa Usafirishaji na Ujenzi wa nchini Malawi, Mh. Francis Kasaila (MB) (kushoto) akikata utepe katika uwanja wa ndege wa kimaifa wa Kamuzu, kuashiria uzinduzi wa ‘route’ mpya ta Lilongwe-Dar ya Shirika la Ndege la Fastjet. Kulia ni Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akishuhudia tukio hilo.
IMG_9696
Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akitia baraka ya uzinduzi huo. Kushoto ni Waziri wa Usafirishaji na Ujenzi wa nchini Malawi, Mh. Francis Kasaila (MB).
IMG_9727
Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati  (kulia) na Waziri wa Usafirishaji na Ujenzi wa nchi Malawi, Mh. Francis Kasaila (MB) (kushoto) kwa pamoja wakikata cake maalum kama ishara ya kupamba uzinduzi huo. Katikati ni Muhudumu wa ndege ya Fastjet, Grace Lukondo.
IMG_9749
Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa ‘route’ mpya ya Lilongwe-Dar na Dar-Lilongwe uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kamuzu.
IMG_9764
Waziri wa Usafirishaji na Ujenzi wa nchi Malawi, Mh. Francis Kasaila (MB) akitoa hotuba wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ‘route’ moya ya Dar-Lilongwe na Lilongwe-Dar katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kamuzu jijini Lilongwe.
IMG_9789
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Bw Wilbrod Kayombo akizungumzia fursa kwa wafanyabiashara baina Tanzania na Malawi  kupitia usafiri huo ambao ni nafuu hata kwa watu wa hali ya chini na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) mara baada ya uzinduzi
IMG_9778
Pichani juu na chini ni baadhi ya maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Malawi, viongozi wa Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Malawi na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo.
IMG_9742e.
IMG_9819
Timu ya waandishi wa habari kutoka Tanzania waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG-20150728-WA0024
Operations Manager wa Modewji blog, Zainul Mzige, akipiga ‘selfie’ kabla ya ndege ya Fastjet kuanza safari yake kutoke Lilongwe-Dar wakati wa halfa ya uzinduzi wa ‘route’ hiyo mpya.
IMG-20150728-WA0026
Wahudumu wa ndege ya Fastjet, Omar Ramadhani na Grace Lukondo wakipata ‘selfie’ ndani ya ndege hiyo mara baada ya kutua jijini Dar ikitokea Lilongwe katika hafla uzinduzi wa ‘route’ hiyo mpya.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...