Friday, July 24, 2015

SERIKALI YAZINDUA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA USALAMA ZA WATU WENYE UALBINO

????????????????????????????????????
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizundua Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hii imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
????????????????????????????????????
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwafafanulia jambo wajumbe wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu, imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
3
Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. Pia alisema Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.
4
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
5
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata hivyo Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...