Wednesday, July 29, 2015

CCM MKOA WA DAR ES SALAAM WAITAKA TUME KUONGEZA VIFAA ILI KUFANIKISHA ZOEZI


Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis ‘Gadafi’ akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………..
Chama Cha Mapinduzi
mkoa wa  Dar es Salaam kimeitaka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza,vifaa na rasilimali watu ili wananchi wengi
waweze kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura bila usumbufu.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu
wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw. Juma Simba Gadafi
  alisema anawashukuru waandishi kwa
ushirikiano waliounesha
  kwenye mkutano
wa kumtambulisha mgombea wa urais 
 kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
uliofanyika tarehe 14 Julai 2015 katika viwanja vya Mbagala Zakheem.
Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza
kwa wingi siku ya tarehe 1 Agosti 2015, kupiga kura za maoni kuchagua wagombea Udiwani
na Ubunge .
 
Katika mkutano huo ambao waandishi wengi walionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua maoni ya  CCM juu ya kuondoka kwa Edward  Lowassa , Katibu wa Siasa na Uenezi  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alisema “Lowasa
aliingia mwenyewe CCM bila shinikizo na kutoka mwenyewe hivyo maamuzi yake hayaifanyi
CCM ishindwe kuendelea kutekeleza majukumu yake”.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...