Sunday, July 19, 2015

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAJITOKEZA KUMLAKI KWA SHANGWE DKT MAGUFULI JIJINI MWANZA


 Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi .
Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe
Magufuli akiwasalimia wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa
jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa,ambao
walijotokeza kumlaki kwa shange na furaha kubwa.Dkt Magufuli amewasili jijini Mwanza akitokea jijini Dar kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla.
 Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwasili jijini Mwanza akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Magufuli yuko jijini Mwanza kujitambulisha kwa Wananchi.
 Mke wa Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt.John Pombe Magufuli,Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake waliojiotokeza kwa wingi kuwapokea,Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.
 Baadhi ya Wananchi wakilikimbiza gari la  Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli kwa shangwe kama waonekanavyo pichani ,wakati Magufuli lipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.
 kuna wengine waliacha kazi kwa muda kama hizi na kuja kwenda kushangilia ujio wa Mh.Dkt John Magufuli
  Wananchi wa Passians wakimpokea na kumshangila Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini.
  Wananchi wa eneo la kona ya Bwiru wakiwa wamezuia  msafara wa Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.
 Wananchi wa eneo la kona ya Bwiru wakiwa wamezuia  msafara wa Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.
    Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa jiji hilo,kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
    Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh John Monela mara baada ya katika uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza.
   Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alisalimiana na wafuasi wa chama hicho wakiwemo viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza,alipowasili katika uwanja wa ndege wa jiji hilo.
PICHA NI MICHUZI JR-MWANZA

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...