Tuesday, July 14, 2015

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA KIWANDA CHA MAFUTA YA ALIZETI SINGIDA


1
 Mkurugezi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary (mwenye kanzu) akimwonesha Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mha. Happiness Mgalula sindano iliyochambuliwa na mashine ya kuchambua uchafu kwenye alizeti inayoletwa kiwandani hapo. Anayetazama ni Mha. Omari Athumani, Mchambuzi Sera Mkuu, Tume ya Mipango.
6
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akionesha dumu la mafuta yanayozalishwa na kiwanda chake tofauti na yale ambayo ni feki ambapo watu wasio waaminifu wanatumia nembo ya kiwanda hicho.
2
 Baadhi ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wakisubiri huduma ya kukamua mafuta kiwandani hapo. Takribani asilimia 80 ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wanataka kukamua mafuta ambapo kiwanda kinawalipisha gharama ya kukamua lakini wao wanaondoka na mafuta yao. Jumla ya wakulima 500 wanaleta alizeti kiwandani hapo.
3
 Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akiwaonesha wajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango machine ya kukamua mafuta ya alizeti (haionekani pichani)
4
Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha kupakia mafuta kwenye madumu wakiendelea kupakia mafuta ya ujazo wa lita tano kiwandani.
5
Ndoo za mafuta ya alizeti kiwandani hapo tayari kupelekwa sokoni.

No comments:

UJIRANI MWEMA KATI YA NGORONGORO NA VIJIJI VYA JIRANI WAZIDI KUIMARISHWA

  Na Mwandishi Wetu Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro anayesimamia Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii, Joas...