Thursday, July 16, 2015

IDD AZAN NA JUMAA MHINA ‘PIJEI’ WACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI NA KAWE

unnamed (1)
Kada wa Chama Cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Jamii UVCCM Dar es Salaam na Kamanda mstaafu wa wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, na Wakili wa Mahakama kuu, Jumaa Mhina ‘Pijei’ akikabidhiwa fomu ya kuomba kuwania Ubunge Jimbo la Kawe,jana jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pijei amejipanga kulikomboa jimbo hilo lililo mikononi mwa wapinzani.
unnamed
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni anayemaliza muda wake, Idd Azzan, akionesha fomu ya kuomba kuwania ubunge wa Jimbo la Kinondoni aliyokabidhiwa jana jijini Dar es Salaam, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
…………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
WAKILI wa Mahakama Kuu nchini, Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Jamii ya Chama Cha mapinduzi (CCM), Dar es Salaam na Kamanda mstaafu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, Jumaa Mhima ‘Pijei’, amechukua fomu za kuwania ubunge Jimbo la Kawe kupitia chama huku.
Pijei, amesema kuwa, hana wasiwasi na wapinzani, lakini akawataka wanachama wa chama hicho Jimbo la Kawe, wasifanye makosa ya kumteua mtu asiyekubalika na wapiga wa kura.
Amesema mwaka 2010, aligombea nafasi hiyo, lakini katika kura za maoni ya CCM hazikutosha, mwaka huu anaamini zitatosha na kulikomboa jimbo hilo lililo mikononi mwa wapinzani.
Kamanda huyo amesema kipaumbele chake ni ajira kwa vijana, elimu, miundombinu ya barabara na umeme na kuwa mafanikio hayo yatakpatikana iwapo atashirikiana kwa karibu na wananchi hivyo, aliomba wananchi kutomwangusha wakati ukifika.
Amesema tayari ametoa ajira kwa vijana kwa kuwapa bodaboda ambazo zimepunguza tatizo la ajira na vitendo vya uhalifu katika jimbo hilo.
Mhina ambaye anafahamika zaidi kwa jina lake la utani la Pijei ambalo pia ndilo la kampuni yake ya ujasiriamali, amesema kipaumbele kingine atakachokitoa ni kuhakikisha anatumia uzoefu wake wa ujasiriamali kwa kuwajengea uwezo wanawake na vijana kwa kuwapa elimu na kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuinua mitaji yao.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...