Thursday, July 16, 2015
DC MAKONDA AKUTANA NA VIJANA WASIO NA AJIRA NA KUWAUNGANISHA, KUBUNI MIRADI YA KIUCHUMI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana ambao hawana ajira wenye elimu tofauti katika viwanja vya Leadres jijini Dar es salaam, ambapo amekutana na vijana hao ili kuzungumza nao kwa ajili ya kutatua tatizo lao lao la ajira .
DC Makonda amesema lengo la kuwaita vijana hao ilikuwa ni kuwakutanisha wafahamiane na wabadilishane mawasiliano lakini pia wataunda vikundi vyao kulingana na taaluma zao na kila kundi litaandika miradi ipatayo mitano ili tuweze kuifanyia kazi kwa kuwatafutia mitaji au ufadhili baada ya miradi yao kubuniwa ,
Ameongeza kwamba mpango huu utapunguza vijana kukaa bila kazi na kuingia katika vishawishi vya mimba kwa wasichana na na matukio yasiyo mema katika jamii. kama vile uhalifu na mengine mengi.
Lakini pia amesema kuna makampuni mengi yameahidi kuchukua vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwani kwa kuwaunganisha vijana hao litakuwa ni jambo rahisi kupata wafanyakazi wa kuajiri , ikiwa ni pamoja na kuchukua vijana watakaofanya kazi kwa kujitolea na baada ya kuonyesha uwezo kazini wao wataajiriwa na mashirika au taasisi husika.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana hao kwenye viwanja vya Leaders
Baadhi ya vijana wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha Chanel Ten.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma
Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment