Wednesday, July 29, 2015

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015  katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai, 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 na kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove aliyesimama nyuma yake pamoja na Mama Salma Kikwete na Mke wa Gavana huyo Mama Cosgrove.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa chakula cha mchana kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.PICHA NA IKULU.


No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...