Mkurugenzi Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko (wapili kulia) akifungua mkutano wa wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono pamoja na wanamuziki na wadau wa filamu kujadili juu ya ushiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo, wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi Leah Kihimbi na wakwanza kulia ni Afisa Utamaduni Bw. Habibu Msami.
Afisa Utamaduni Bw. Habibu Msami (kulia) akitoa ufafanuzi wakati wa mkutano wa wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono pamoja na wanamuziki na wadau wa filamu kujadili juu ya ushiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
Mjasiriamali wa kazi za sanaa za mikono na Mkurugenzi kutoka Bab Ally Tailoring Mart Bibi. Amina Hamza (aliyesimama) akichangia wakati wa mkutano wa wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono pamoja na wanamuziki na wadau wa filamu kujadili juu ya ushiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) jana jijini Dar es Salaam.
Mjasiriamali wa kazi za sanaa za mikono na mwanzilishi wa Kindai Art Centre Mwenge Handcraft Village Bibi. Carolyne Kessy (aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono pamoja na wanamuziki na wadau wa filamu kujadili juu ya ushiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi (katikati) akizungumza na wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono pamoja na wanamuziki na wadau wa filamu wakati wa mkutano wa kujadili juu ya ushiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko, na kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo.
Baadhi ya wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono pamoja na wanamuziki na wadau wa filamu wakifuatilia kwa makini mambo mbalimbali yaliyokua yakijadiliwa katika mkutano wa kujadili juu ya ushiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) jana jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………….
Habari Picha-Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono, wanamuziki pamoja na wadau wa filamu nchini wametakiwa kuzingatia ubora wa kazi hizo ili kuweza kupeperusha bendera ya Tanzania nchi jirani na duniani hivyo kuleta mabadiliko katika tasnia ya sanaa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi kutoka Modern Natural Herbs Bw. Iddi Kuziwa wakati wa mkutano wa wajasiriamali wa kazi za sanaa za mikono pamoja na wanamuziki na wadau wa filamu kujadili juu ya ushiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) jana jijini Dar es Salaam.
“Bidhaa za sanaa kutoka nchini Tanzania zinapendwa sana na watu wengine kutoka nchi za Afrika na duniani kote hivyo hatuna budi kuandaa bidhaa nyingi na zenye ubora tutakazoonyesha wakati wa tamasha la JAMAFEST ili kuweza kuleta mabadiliko katika tasnia ya sanaa, kushindana na wadau wa sanaa kutoka nchi nyingine na kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania” alisema Bw. Kuziwa.
Akitoa mwelekeo wa Tamasha hilo Mkurugenzi Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko amesema kuwa tamasha kama hili la JAMAFEST linasaidia kutoa nafasi kwa wadau wa sanaa kujifunza kutoka nchi nyingine hivyo kuboresha zaidi kazi za sanaa za Tanzania kwani utamaduni husaidia katika kukuza uchumi kama utapewa nafasi.
Prof. Mwansoko amewataka wajasiriamali na wadau wa sanaa kutumia fursa hiyo kujionyesha kujitangaza na kuuza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ili kuweza kuteka soko la Afrika Mashariki kwa kuwa na bidhaa nzuri zaidi za sanaa.
Naye Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Habibu Msami amewataka wadau wa kazi za sanaa nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha hilo na kuwa na umoja ili kuweza kuleta mafanikio nchini.
Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) lenye kauli mbiu ‘kufungua uwezo wa kiuchumi wa utamaduni na ubunifu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki’ linatarajia kufanyika kwa mara ya pili Agosti 2 hadi 9 mwaka huu nchini Kenya baada ya tamasha la kwanza kufanyika mwaka 2013 mjini Kigali nchini Rwanda.
Tamasha hilo limedhamiria kuonyesha sanaa za jukwaani, maonyesho ya bidhaa mbalimbali za kiuchumi, makongamano, michezo na sanaa za watoto, kutoa nafasi kwa washiriki kutembelea vivutio asilia vya utamaduni vilivyopo nchini Kenya pamoja na kuwa na soko la tamasha la kuuzia bidhaa za kiutamaduni kutoka nchi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment