Thursday, July 23, 2015

JOSHUA NASSARI ACHAGULIWA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

`Aliekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha,Joshua Nassari akizungumza namna alivyotekeleza ahadi zake katika kipindi kilichopita wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo uliofanyika kwenye Mji mdogo wa Usa River ambao  alichaguliwa bila kupingwa ili kupeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Wanachama wa Chadema wakipiga kura za maoni kwaajili ya kumchagua mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki katika Mji Mdogo wa Usa River,Joshua Nassari alipata kura 387  na kura 2 za hapana.

Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo

Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini ambaye alikua Mbunge wa Chadema jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Israel Natse(kulia)na Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalist Lazaro wakimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari(kati)baada ya kutangazwa mshindi.

WanaChadema wakifatilia kwa makini mkutano mkuu wa jimbo ambao pia ulifanya uchaguzi wa wabunge wa viti Maalumu,Rebeca Mngodo aliibuka mshindi wa kwanza kwa kupata kura 62 kati ya wagombea watano.
Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo Mkuu wa jimbo uliofanyika katika Mji Mdogo wa Usa River.

Aliekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha,Joshua Nassari(kulia) akizungumza jambo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,Dk Elly Macha.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...