Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Mkoa wa Arusha ,Catherine Magige akizungumza jana katika mkutano wa wagombea Ubunge 12 kupitia chama cha mapinduzi waliofanya ziara ya kujinadi kwa wananchama pamoja na wananchi kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho jana katika mtaa wa kati(CCM Mkoa),ambapo hivi karibuni Catherine aliibuka ushindi wa kishindo kwa kura 409 kati ya kura 560 huku anayemfwatia akipata kura 248.
Habari picha na Pamela Mollel
Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige akisalimiana na wanachama wa chama hicho jana jijini Arusha,Aliwatoa rai kwa wananchi na wananchama wa chama cha mapinduzi kumuunga mkono mgombea Urais Dk.John Pombe Magufuli kwani ndio chaguo la CCM,huku pia akisisitiza wanaccm kuchagua kiongozi kwanzia ngazi ya udiwani,ubunge anayekubalika ndani ya CCMna nje ya CCM.
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha, Mayasa Kimbau ambaye pia ni mratibu wa Mkoa akiteta jambo na Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha jana katika mtaa wa kati (CCM Mkoa) wakati wa ziara ya watia nia wa chama cha mapinduzi wakijitambulisha na kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama hicho katika nafasi ya Ubunge.
No comments:
Post a Comment