Thursday, July 16, 2015

DAVIS MOSHA ATANGAZA RASMI NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI

Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mjini wakiwa katika uwanja wa Mashujaa katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mtangaza nia wa nafasi ya Ubunge wa jimbo la Moshi mjini ,Davis Mosha.
Mtangaza nia ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha ,akiwa na meneja kampeni wake Voctor (kushoto kwake pamoja na Goodluck Moshi.
Baadhi ya makada waliofika katika uwanja huo.
Msanii wa filamu Tanzania Stephen Mengere maarufu kama Steve Nyerere alikuwa ni mmoja wa makada wa chama hicho waliofika kutoa hamasa katika mkutano  huo uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa.
Baadhi ya kina mama waliofika katika mkutano huo.
Baadhi ya vijana wakiwa na mabango yao waliofika katika mkutano huo.
Wasanii wa Bongo Movie walipamba mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wa Moshi mjini waliofika katika mkutano huo wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Kada wa Chama cha Mapinduzi,Octavian akimtambulisha mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha kwa wakazi wa Moshi waliofika katika uwanja wa Mashujaa.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.
Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akisalimiana na wakazi wa Moshi waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa.
Davis Mosha akizungumza na waandishi wa habari marabaada ya mkutano wake wa kutangaza nia.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge Davis Mosha akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara mjini Moshi waliofika katika mkutano huo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...