Monday, July 27, 2015

MUUNGANO WA JUMUIYA ZA MARADHI YASIYO AMBUKIZA ZANZIBAR ZATOA TAALUMA YA MARADHI YASIYO AMBUKIZA

 mail.google.com
Katibu wa Taasisi ya  Zanzibar Heart Foundation Sururu Abass Othman akizungumza na wananchi  wa shehia za Muembemakumbi, Karakana na  Chimbuni waliofika kuchungaza Afya zao.
Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar
mail.google.comn
Mratibu wa Muungano wa Taasisi zinazoshughulikia maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (ZNCDA) Omar Abdalla Ali akiwaelimisha wananchi waliofika kituo cha Afya Karakana kuchunguza afya juu ya maradha ya maradhi hayo na njia bora za kujikinga.
f
Muuguzi wa Kituo cha Afya Karakana  Mere Hamad Jadi akiwapima wananchi maradhi ya sindikizo la damu  wakati wa zoezi hilo lililofanyika Kituo cha Afya cha Karakana nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
mail.google.comv
…………………………………………………………….
Na RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR.
Muungano wa Taasisi zinazoshughulikia   maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (ZNCDA) umeishauri Serikali na Mashirika wahisani kuelekeza nguvu zao katika mapambano  dhidi ya  maradhi hayo  kwa vile hivi sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya wananchi  kuliko maradhi mengine yoyote Zanzibar.
Mratibu wa ZNCDA Omar Abdalla Ali alitoa ushauri huo wakati wa zoezi la  kuwapima  afya  wananchi wa shehia za Karakana, Chimbuni na Muembemakumbi, Mkoa Mjini Magharibi Unguja,  lililofanyika Kituo cha Afya cha Karakana.
Alisema maradhi ya Sindikizo la damu, Kisukari na Saratani  yamejitokeza kuwa tishio  kwa wananchi  kutokana na uelewa  wao mdogo juu ya  maradhi hayo na wengi kutokuwa na mwamko wa kupima afya zao.
Alizitaja sababu zinazochangia kuongezeka maradhi yasiyoambukiza  kuwa ni mabadiliko ya  mfumo wa maisha ambao wananchi   hupenda zaidi starehe kuliko kujituma, uvutaji sigara,  ulevi wa kupindukia  na kutumia chakula cha makopo kilichotiwa kemikali.
Akitowa takwimu ya maradhi hayo, Omar  alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2011  asilimia 33 ya wananchi wa Zanzibar wanakabili na  sindikizo la damu na  asilimia nne wanamaradhi ya kisukari na taarifa  kutoka Hospitali ya Ocean Road Dar es Salaam zinasema kuwa  kila mwaka wanapokea kiasi cha wagonjwa 1000 wa magonjwa ya saratani kutoka Zanzibar.
Aliongeza kuwa saratani ya matiti na shingo ya kizazi kwa akinamama na tenzi dume  kwa wanaume  zinaongoza  kati ya wagonjwa wanaopelekwa huko kupatiwa matibabu.
Alisema taarifa hizo zinatisha kutokana na idadi ndogo ya wananchi wa Zanzibar na ni sababu iliyopelekea ZNCDA kufanya juhudi  ya kutoa taaluma kwa wananchi, kuwapima afya ndani ya shehia zao na kuwapa ushauri unaofaa wa kujikinga na maradhi hayo.
Aliwataka wananchi kuanzisha  utamaduni wa kupima afya  mara kwa mara  ili kujua  afya zao mapema  badala ya  kusubiri kuathiriwa na maradhi ndipo wakimbilie Hospitali.
“Maradhi yanapogundulika mapema ni rahisi kuyatibu lakini unaposubiri mpaka yakakuathiri inakuwa  vigumu kuyatibu pimeni afya zenu kila wakati, ” alisisitiza Mratibu wa ZNCDA.
Aliwashauri viongozi wa Serikali za mitaa, wabunge ,wawakilishi na madiwani, kuwasaidia wananchi  kwa kuwawekea vifaa vya kupima afya zao katika sehemu wanamoishi kwa vile vifaa hivyo havina gharama kubwa.
Jumla ya wananchi 174 kutoka shehia hizo tatu walipata nafasi ya kuangaliwa afya zao na maradhi ya sindikizo la damu yamegundulika  kuongoza katika shehia hizo.

No comments: