Ilikiwa ni safari ngumu lakini yenye mafunzo mengi nikiwa nimepanda kwenye boti ya Doria wakati wa msafara wa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na msafara wake tukitokea Nyamisati kuelekea Mafia ambapo katibu Mkuu huyo yupo katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa akikagua miradi ya mendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Nilipangiwa kupanda boti hii ya mwendo kasi ili kupata taswira za msafara kwa ujumla na hizi ndiyo tawira zenyewe endelea kuperuzi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-PWANI)Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jamno pamoja na wabunge wa Mafia Abdulhimid Shah kulia na Abdull Marombwa wakati Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnnauye alipokuwa akiwaaga wananchi katika mji wa Nyamisati wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ukielekea Mafia wakati akiwa katikaziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo. Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnnauye akiwa pamoja na wananchi mara baada ya kupanda kwenye boti kuelekea kisiwani Mafia jana.Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge wa Mafia Mh. Abdulhimid Shah wakipungia mkono wananchi mara baada ya boti hiyo kuondoka katika pwani ya Nyamisati.Boti ikikata mawimbi baharini huku bendera za CCM zikipepea.Mawimbi makali kidogo lakini ndiyo mwendo wenyewe.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakiwa kwenye mtumbi kuelekea pwani ya Mafia baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kiwani humo jana.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakiwa kwenye mtumbi kuelekea pwani ya Mafia baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kiwani humo jana. Katikati anayepunga mkono ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe MlaoKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi pamoja na mbunge wa Mafia Mh. wakiwa Mafia Mh. Abdulhimid Shah kwenye pwani ya Mafia baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kisiwani humo jana.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitoa burudani mara baada ya kwasili kisiwani Mafia jana.Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika uwanja wa stendi ya mabasi mjini mafia jana.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi jana mjini Mafia.Mh. Abdulhimid Shah mbunge wa Mafia akiwahutubia wananchi wa jimbo lake.Naibu Waziri wa Nishati nishati na madini Mh. Charles Kitwanga akiwahutubia wananchi wa Mafia na kuwaelezea mipango ya serikali juu ya huduma ya umeme katika kisiwa hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN UAPISHO WA RAIS WA MSUMBIJI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa zamani wa Msumbiji, Joaquim Chissano katika sherehe za kumwapisha Rais wa Msumbiji...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment