Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mama Veronica Simba wa Majengo Mombo wilayani Korogwe wakati alipomtembelea jimbo la Korogwe vijijini linaloongozwa na Mh. Steven Ngonyani Maarufu kama Prof. Maji Marefu, katika mradi wake wa kufundisha wanafunzi wa ushonaji wa nguo akiwa katika ziara yake mkoani Tanga akikagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuhimiza huai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MOMBO-KOROGWE)Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo wakati alipomtembemea mama Veronica Simba katika eneo la majengo mjini Mombo leo huku wanafunzi wa mama Veronica Simba wakifurahia tukio hilo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo wakati alipomtembemea mama Veronica Simba katika eneo la majengo mjini Mombo huku mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Mh. Steven Ngonyani akifurahia.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi katika wa maabara katika shule ya sekondari ya Chekereni mjini wilayani Korogwe.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu kulia na Mrisho Gambo Mkuu wa wilaya ya Korogwe wakati alipowasili katika shule ya sekondari ya Cherereni Mombo.Waandishi wa habari waliokatika msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Said Mwishehe wa Jambo Leokulia na David John wa Majira wakizungumza na wanafunzi katika shule ya sekondari Machewa.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani alipokuwa akitoa maelezo kuhusu sekondari ya Mashewa wilayani Korogwe, Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Ndugu Mrosho Gambo.Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akimimina zege wakati akishiriki katika ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Mashewa huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuhudia tukio hilo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya w atendaji wa serikali wakati alipowasili katika shule ya sekondari ya Chekereni kukagua mradi wa ujenzi wa maabara ya shule hiyo.Mmoja wa wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Mombo leo Bw.Mageda Hamza akiuliza swali katika mkutano huo.Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu katikati ni Mnec wa wilaya ya Korogwe vijijini Ndugu Edmund MndolwaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mgolole kama ishara ya heshima ya wasambaa kumkaribisha mgeni shujaa kwao wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo.Wananchi waliohudhuria katika kutano huo wakinyoosha mikono yao juu kama salamu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman KinanaMmoja wa masjhabiki wa CCM akionyesha alama ya vidole viwili juu kama ishara ya kukubali jambo katika mkutano huo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakipungia wananchi mikono wakati alipowasili katika eneo la mkutano wa hadhara mjini Mombo Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa akizungumza na wana Mombo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mombo jana.Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akizungumza na wapiga kura wake mjini Mombo Korogwe jana.Wananchi wakinyanyua mikono yao juu wakati wa mkutano huo.Baadhi ya wasichana wa kimasai wakiwa katika mkutano huo. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mombo jana.
No comments:
Post a Comment