Friday, September 26, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ALIMA KWA POWER TILLER MAHENGE KOROGWE

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivua viatu vyake tayari kwa kushiriki kulima shamba la la mpunga katika mradi wa Umwagiliaji wa kata ya Mahenge ambao taarifa ya mradi huo imesema maendeleo yake ni mazuri na sasa wakulima wa mashamba hayo wanaweza kuvuna mpunga kiasi cha zaidi ya  tani nne kutoka uzalishaji wa tani mbili tu hapo awali, Katibu Mkuu yuko katika ziara ya mikoa mitatu ambapo alianzia katika mkoa wa Pwani na sasa yuko mkoani Tanga kabla ya kuelekea mkoani Iringa ambapo atamalizia ziara yake akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM  ya mwaka 2010, Katika ziara hiyo pia Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- KOROGWE)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kilimo cha mashamba ya mpunga katika shamba la mradi wa umwagiliaji la Mahenge wilayani Korogwe kwa kutumia Power Tiller3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kilimo cha mashanmba ya mpunga katika shamba la mradi wa umwagiliaji la Mahenge wilayani Korogwe kwa kutumia Power Tiller, wengine ni wafanyakazi wa shamba hilo wakishuhudia tukio hilo.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi  katika kilimo cha mashamba ya mpunga katika shamba la mradi wa umwagiliaji la Mahenge wilayani Korogwe kwa kutumia Power Tiller5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinawa miguu baada ya kushiriki katika kazi hiyo.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi kushoto na kada wa CCM Dk. Edmund Mndolwa  mara baada ya kushiriki katika kilimo cha mashamba ya mpunga katika shamba la mradi wa umwagiliaji la Mahenge wilayani Korogwe kwa kutumia Power Tiller7Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mahenge wilayani Korogwe.8Mbunge wa jimbo la Korogwe mjini Mh. Yusuf Nasir akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mahenge mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kukagua ujenzi wa zahanati hiyo, kushoto ni Henry Shekifu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo wakishiriki kazi ya kusafisha soko la Sabasaba.10Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na wananchi katika tawi la CCM la Kwamsisi Juu. 11Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na Daniel Chongolo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano CCM.13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa Maabara ya shule ya sekondari ya Old Korogwe kushoto anayeshuhudia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.14Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa CCM uliofanyika kwenye uwanja shule ya Msingi Mazoezi.15Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mazoezi mjini Korogwe.16Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mazoezi mjini Korogwe.17Baadhi ya wananchi wakinyanyua mikono juu wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia mjini Korogwe .18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi mjini Korogwe 19Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.20Mbunge wa jimbo la Korogwe mjini Mh. Yusuf Nasir akiwahutubia wapiga kura wake mjini Korogwe.21Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Mazoezi mjini Korogwe.22Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Bw. Athman Said  aliyehamia CCM akitokea chama cha CUF ambapo alitumikia chama hicho  kama Kaimu Katibu wa wilaya ya Korogwe.23Bw. Athman Said  aliyehamia CCM akitokea chama cha CUF akitoa ushuhuda wake mara baada ya kupokea kadi yake Athman Said  alitumikia chama hicho  kama Kaimu Katibu wa wilaya ya Korogwe.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...