Monday, September 22, 2014

JAMII YA HAMASISHWA KUJITOLEA KUHUDUMIA WAHANGA WA AJALI ZA BARABARANI

CK1 Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo (katika) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua maonyesho ya Saba ya Magari yajulikanayo kama Atofest jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Biafra. Kulia ni Msaidizi Binafsi wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Deodatus Timothy Ndunguru na kushoto ni Mratibu wa maonyesho hayo Bw. Ally Nchahage.
CK2Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika banda la Jaffarais Car Wash wakisubiri wateja kwa ajili ya kuwaoshea magari ikiwa ni mchango kwa ajili ya kusaidi wagonjwa walioko hospitali ya Taifa Muhimbili watokanao na ajari za barabarani. Tukio hili limefanyika jana katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam.
CK2aMsanii Singo Mtambalike aka Rich Rich (aliyeshika mpira wa maji) na msanii wa kike Bi. Kajala Masanja (  aliyeshika ndoo) wakiosha gari la mteja aliyefahamika kwa jina la Furaha Mansoor (hayupo pichani) mara baada ya kufikia makubaliano ya kumuoshea gari mteja kwa ikiwa ni mchango wa kusaidia wahanga wa ajali za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wasanii hao waliosha gari hilo kwa gharama ya shilingi laki tano za kitanzania.
CK2b Mkurugenzi waKampuni ya SBP Bw. Furaha Mansoor (katikati) akiwakatika picha yapamoja na wasanii Singo Mtambalike aka Rich Rich (kushoto) na Kajala Masanja (kulia) mara baada ya wasanii hao kumaliza kumuoshea gari lake wakati wa maonyesho ya magari na zoezi la uchangiaji wa hiari kwa wahanga wa ajali za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Biafra 
CK2c Wasanii Johari Chagula (anayepaka sabuni) na Monalisa (  aliyeshika mpira wamaji) wakiosha gari la mteja aliyefahamika kwa jina la Feisar (hayupo pichani) mara baada ya kufikia makubaliano ya kumuoshe gari mteja huyo kwa ikiwa ni mchango wa kusidia wahanga wa ajari za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
CK3 Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mahusiano wa Benki ya Afrika Tawi la Tanzania (BOA Bank) Bi. Gereta Gonga alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo  jijini Dar es Salaam.
CK4. Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akifurahia zawadi ya Kikombe aliyopewa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Kuunganisha wauzaji na wanunuzi wa magari Tanzania kupitia mtandao wa cheki.co.tz Bw. Mori Bencus jijini Dar es Salaam. Kampuni ya ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ya saba ya Atofest ambapo wameingia kwa mara ya kwanza katika biashara hapa nchini Tanzania mwaka 2014 wakiwa na lengo la kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na kwa wakati.
CK5 Gari lenye uwezo wakuhimili katika maeneo yasiyo na barabara zauhakika likiendeshwa katikati ya dimbwi la matope kuonyesha uimara wake,hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam katika maonyeshi ya magari yanayonedelea katika viwanja vya Biafra Kinondoni.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...