Walimu waliokuwa wakiendesha mafunzo kwa watoto hao wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Beatha Qambayot, Zilpa Masunga, Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Maalumu Tanzania, Frank Macha na Alphonsia Mwairafu.
Walimu hao wakiwa wameshika mipira ya kufundishia.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)
Watoto wenye ulemavu wa akili wakiwa katika picha na wazazi, pamoja na walimu wao baada ya kumaliza mafunzo ya mwezi mmoja ya Olimpiki Maalumu Tanzania yaliyofikia tamati wilayani Temeke Dar es Salaam.
Mmoja wa wazazi akiwa na watoto hao.
Wazazi na walezi wakiwaelekeza watoto wao mchezo wa kurusha kitu na kudaka.
Wazazi na walezi wakiwaelekeza watoto wao mchezo wa kurusha kitu na kudaka.
Wazazi wakiimba pamoja na watoto wao.
Wakufunzi wa mafunzo hayo wakiwaelekeza watoto hao kutembea huku wakiwa wameweka kitu kichwani bila ya kukishikilia.
Wazazi wakiwa na watoto wao kwenye mafunzo hayo.
Watoto hao wakigaiwa maputo kabla ya kuanza kuimba.
Mmoja wa watoto hao akicheza mchezo wa kupita katika ringi. Kulia na kushoto ni wakufunzi wa mafunzo hayo.
Hadija Balila mmoja wa wazazi mwenye mtoto mlemavu (kulia), akihojiwa na wanahabari kuhusu faida ya mafunzo hayo.
Watoto hao wakicheza mchezo wa kukimbia na kuweka mpira katika kikapu. Mchezo huo unawaandaa kuja kucheza mchezo wa kikapu.
Wakufunzi wa mchezo huo wakimtuza Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Maalumu Tanzania, Frank Macha kitenge kwa mchango wake wa hali na mali kwa kuwawezesha watoto hao kupata mafunzo hayo.
Mkufunzi Zilpa Masunga, akicheza na watoto hao.
Dotto Mwaibale
JAMII nchini imetakiwa kutowaficha watoto wenye matatizo ya akili badala yake wawashirikishe katika michezo mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa uelewa na kuimarisha viungo vyao.
Mwito huo umetolewa na Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Malaamu Tanzania, Frank Macha Dar es Salaam jana wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja ya olimpiki ya watoto hao kutoka wilaya ya Temeke.
“watoto wenye ulemavu wanapojumuika na watoto wenzao katika mafunzo ya michezo upata faraja na viungo vya miili yao ulainika hivyo kuwaongezea uwezo wa kutembea na changamka tofauti na mtoto ambaye hukosa mazoezi yatokanayo na michezo” alisema Masha.
Alisema mtoto anayefungiwa ndani kutokana na ulemavu wake mara nyingi anakuwa apendi kujumuika na watu wengi tofauti na mtoto ambaye anashirikishwa na wenzake katika michezo ambayo pia inawakutanisha wazazi wa watoto hao.
Masha alisema mafunzo hayo ya olimpiki maalumu Tanzanaia yaoanza mwanzoni mwa mwezi huu yamewashirikisha watoto 150 katika wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam ambap0 kwa wilaya ya Kinondoni ilifanyika Kawe, Ilala, Ukonga na Temeke katika Shule ya Msingi ya Wailes.
Alisema watoto walioshiriki olimpiki hiyo ni kuanzia miaka mitatu hadi nane na kuwa walikuwa wakipatiwa mafunzo ya michezo mbalimbali na walimu wenye utaalamu wa kufundisha watoto wenye matatizo hayo ya akili.
Hadija Balila mmoja wa wazazi mwenye mtoto mlemavu alisema kuwakutanisha watoto hao katika mashindano kama hayo kunawasaidia kuchangamka na kuwafanya nao wajione kama watoto wengine na akatoa mwito kwa wazazi na walezi wenye watoto wa aina hiyo wasiwafiche ndani kwa kuona aibu.
No comments:
Post a Comment