Shirika la ndege la Etihad Airways litaongeza safari zake barani Afrika kwa kuzindua safari mpya ya kila siku ya mji wa Dar es Salaam
ABU DHABI, United Arab Emirates,September 23, 2014/ — Shirika la ndege la Etihad Airways (http://www.etihad.com), ambali shirika la ndege la kitaifa la Umoja wa Falme za Kiarabu, litaongeza safari zake barani Afrika kwa kuzinfua safari mpya ya kila siku Mjini Dar es Salaam, mji mkubwa zaidi Tanzania.
Download Etihad New Routes 2015 Map: http://www.apo-mail.org/Etihad-New-Routes-2015-map.PDF
Safari hizi za ndege kati ya Abu Dhabi na Dar es Salaam, zitaanza tarehe 1 mwezi Desemba 2015, zikiendeshwa kwa kutumia ndege ya Airbus A320 yenye viti 16 vya kitengo cha Biashara na 120 vya kitengo cha Uchumi.
Dar es Salaam itakuwa kituo cha 110 cha Etihad Airways duniani kote, na kituo cha 11 barani Afrika na Bahari ya Hindi. Ratiba hii ya kila siku itatoa njai mbili za uunganishwaji katika kitovu cha Etihad Airways mjini Abu Dhabi, pamoja na uunganishaji rahisi wa safari zingine za vituo 45 maarufu katika Mashariki ya Kati, Ulaya, Bara Dogo la India, Asia Kaskazini na Kusini-Mashariki, na Australasia.
Hasa, inatarajiwa kwamba mahitaji ya njia hii mpya yataongezwa na wasafiri wengi wa kibiashara na utalii, pamoja na viwango vya mizigo, kati ya maeneo ya Afrika Mashariki na Bara Dogo la India na China.
James Hogan, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Etihad Airways, alisema:”Dar es Salaam ni njia muhimu kwenye mtandao mkuu wa Etihad Airways. Inaimasharisha kuwepo kwetu Afrika, na kusaidia uhusiano wa karibu wa kibiashara kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Tanzania.”
Umoja wa Falme za Kiarabu ni mbia mkuu wa kibiashara wa Tanzania katika eneo la GCC. Kati ya 2007 na 2012, biashara kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Tanzania imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 350 hadi Dola milioni 761 za Marekani.
Aliendelea kusema, “Afrika ina uchumi unaokua haraka sana duniani kote, na uzinduzi wa njia hii mpya pia unaongeza ufikiaji na utiririkaji wa baishara na utalii pande zote mbili kati ya bara hilo na vituo msingi katika mtandao wetu mkuu, unaongeza watalii kutoka nje, unahamasisha uwekezaji, na utatoa ajira zinazohitajika sana barani humu.”
Tanzania ni nchi ya siti barani Afrika kwa idadi ya watu (watu milioni 51), ambapo zaidi ya watu milioni nne wanaishi katika mji mkublwa zaidi, Dar es Salaam. Sehemu kubwa ya jamii hiyo inajumuisha wanabiashara na wamiliki wa biashara ndogondogo ambao asili ya familia zao ni Mashariki ya Kati na Bara Dogo – maeneo ya dunia ambayo wakazi wa pwani ya Tanzania wamekuwa na uhusiano mkubwa wa kibiashara nao.
Nchi hii pia inakua haraka, na kwa sasa ina takriban Dola bilioni 19 za Marekani katika miradi ya miundombinu ya usafiri na huduma inayopangwa. China imejihusisha pakubwa katika kugharamia miradi hiyo mikubwa, na inaendelea kuwa mbia wa kwanza kibiashara na nchi hii ya Afrika Mashariki, biashara kati ya nchini hizi mbili ikikuwa kwa Dola bilioni 3.7 za Marekani katika 2013.
Katika 2013, Tanzania pia ilitajwa kama moja ya maeneo yanayowavuti watalii sana duniani kote, na imebarikiwa na vivutio vingi vya watalii wa kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama za kitaifa za Serengeti, na kisiwa cha viungo cha Unguja.
Uchumi wa Tanzania ni wa pili katika Afrika Mashariki, na Dar es Salaam ndio njia ya kimkakati ya usafirishaji wa bidhaa na biashara katika nchi sita jirani zisizokuwa na bahari za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Rwanda na Burundi.
Download the table “Ratiba ya Etihad Airways ya safari za ndege za Dar es Salaam, kuanzia tarehe 1 Desemba 2015″: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/photos/140923sw.png
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Damian James, Mawasiliano ya Shirika ya Etihad Airways
Saa: +971 (0) 2 511 1035 / Barua Pepe: DJames@etihad.ae
Kuhusu Etihad Airways
Shirika la ndege la Etihad Airways (http://www.etihad.com) lilianza shughuli zake mwaka wa 2003, na mnamo 2013 lilikuwa limewasafirisha watu milioni 11.5. Kutoka makao yake mjini Abu Dhabi Etihad Airways husafirisha abiria na mizigo kwa vituo 110 vilivyoko au vilivyotangazwa katika Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika hili la ndege lina msafara wa ndege 104 za Airbus na Boeing, na zaidi ya ndege 200 ambazo zimeagizwa, ikiwa ni pamoja na Boeing 787 71, Boeing 777-X 25, Airbus A350 62 na Airbus A380 10. Etihad Airways ina uwekezaji katika airberlin, Air Seychelles, Virgin Australia, Aer Lingus, Air Serbia na Jet Airways, na iko katika mchakato wa kurasimisha uwekezaji katika Alitalia na Etihad Regional* yenye makao yake Uswisi. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.etihad.com
*Inaendeshwa na Darwin Airline
SOURCE
Etihad Airways.
No comments:
Post a Comment