Tuesday, September 30, 2014

BALOZI WA JAPAN ZIARANI WILAYANI MONDULI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimkaribisha wilayani Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh.  Masaki Okada wakati alipowasili wilayani humo juzi Jumapili Septemba  28,2014 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi hiyo.Balozi huyo aliahidi kusaidia vifaa vya  kisasa katika hospitali mpya ya kisasa inayojengwa wilayani humo.
Meneja wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akimkaribisha  Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni  kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli,Bw. Twalib  Mbasha.
Balozi wa Japan nchini,Mh. Masaki Okada (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha (kulia) na Meneja wa  Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema alikofikia balozi huyo na 
ujumbe wake katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI DUA MAALUM KUMUENZI HAYATI KARUME, MIAKA 54 BAADA YA KUUAWA KWAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan , jana tarehe 07 Aprili 2026 aliungana na viongozi mbalimbali pamoja na wananch...