Friday, September 19, 2014

Taarifa Kwa Umma Kutoka Makao Makuu ya Jeshi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Kuhusu Kupandishwa Vyeo Kutoka Brigedia Jenerali Kuwa Meja Jenerali

 
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja Jenerali Simon Mumwi, Makao Makuu JWTZ Upanga jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja Jenerali Gaudence Milanzi 
 
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja JeneraliVenanceMabeyo.
 
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kushoto akimvisha cheo kipya Meja Jenerali Ndetaulwa Zakayo Makao Makuu JWTZ Upanga jijini Dar es salaam.
Meja Jenerali James Mwakibolwa mara baada ya kuvishwa cheo kipya na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange hayupo pichani. 
---
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mujibu wa Kanuniza Majeshi ya Ulinzi, Aya ya 7.01 Kifungu cha (3) amewapandisha cheo Maafisa Saba (7) kutoka Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali kuanzia Septemba 12, 2014. Waliopandishwa cheo ni kama ifuatavyo:-

  1. Brigedia Jenerali Gaudence Milanzi kuwa MejaJenerali.
  2. Brigedia Jenerali James Mwakibolwa kuwa Meja Jenerali.
  3. Brigedia Jenerali Ndetaulwa Zakayo kuwa Meja Jenerali.
  4. Brigedia Jenerali Venance Mabeyo kuwa Meja Jenerali.
  5. Brigedia Jenerali Simon Mumwi kuwa Meja Jenerali.
  6. Brigedia Jenerali Issa Nassor kuwa Meja Jenerali.
  7. Brigedia Jenerali Rogastian Laswai kuwa Meja Jenerali.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amewavisha cheo cha Meja Jenerali kwa niaba ya Rais. Sherehe hizo fupi zitafanyika Makao Makuu ya Jeshi Upanga Dar es Salaam.

Aidha, Meja Jenerali Milanzi, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) kufuatia nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkuuwa Chuo hicho Luteni Jenerali Charles Makakala ambaye amestaafu. Kwa mujibu wa sharia baada ya kulitumikiaTaifa kwa uaminifu na uadilifu wa hali ya juu.

Imetolewana

Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963

No comments:

WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA KAMPENI YA ‘PERFOM AND INFORM’

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, akizungumza katika Kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika leo Januari ...