Tuesday, September 23, 2014

MAZIKO YA MAREHEMU IDDI PANDU HASSAN

IMG_6055[1] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ALhaj Dk. Mohamed Gharib Bilali waliungana na wananchi mbali mbali katika maziko ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan aliyezikwa kijijini kwao Kipunguni Makunduchi jana,{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
IMG_6039[1]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nnne kulia) akiwepo na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume wakijumuika na waisalmu katika kumswalia Marehemu  aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan katika Msikiti wa Mchekeni Magomeni Mjini Zanzibar jana na Kuzikwa kijijini kwao Makunduchi, {Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]IMG_6035[1]Baadhi ya akina mama walioshiriki katika mazishi ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu  Iddi Pandu Hassan nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja,{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]IMG_6026[1]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofika nyumbani kwa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwapa pole wafiwa jana kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]IMG_6034[1]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Ndugu wa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipofika kuwapa pole wafiwa nyumbani kwa marehemu Magomeni Mjini Zanzibar  jana kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...