Saturday, September 27, 2014

KAMATI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA ZAPENDEKEZA KUWEPO KUZUIA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI

SHABaadhi ya Kamati za Bunge Maalum la Katiba zimependekezwa kuwepo kwa Ibara mpya inayohusu kuanzishwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi katika sura ya 15 ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Hayo yamebainika jana wakati wa uwasilishaji wa taarifa  za Kamati Namba Moja hadi Kamati Namba Kumi na Mbili za Bunge hilo kuhusu uhakiki wa Rasimu hiyo  uliofanyika  kwenye kikao cha arobaini na tatu kilichofanyika mjini Dodoma.
Taarifa hizo,ambazo zimewasilishwa na baadhi ya wenyeviti wa Kamati hizo na baadhi ya wajumbe kutoka 201  waliopewa ridhaa  za kuwasilisha.
Baadhi ya Kamati  za Bunge hilo,ambazo zimependekeza suala ni  Kamati  namba 1,2,5,3, 6,8.9,10 na 12.
Akizungumzia kuhusu suala hilo Makamu  Mwenyekiti wa Kamati Namba Mbili, Shamsa Mwangunga alisema  katika Kamati yake  baada ya kupitia na kujadiliana suala la kuongeza ibara inayohusiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi.
“ Katika sura ya 15 ninayohusu Taasisi za Uwajibikaji, Kamati inapendekeza kuwe na Ibara inayoanzisha Taasisi hiyo na mambo mengine ya utafiti, uchunguzi na n.k( nakadhalika) yawekwe kwenye sheria husika,” alisema Mwangunga.
Akisoma taarifa ya Kamati Namba Sita ya  Bunge Maalum la Katiba, mjumbe wa Bunge hilo, Charles Mwaijage alisema katika  kukabiliana na tatizo la rushwa na uhujumu uchumi, Bunge litatunga sheria juu ya kuwepo kwa taasisi  hiyo, ambapo itaainisha majukumu ya msingi ya taasisi hiyo katika utafiti, uchunguzi wa makosa kuchukua hatua stahili dhidi ya watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...