Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.
Wananchi wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83 vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vyumba vya maabara za shule ya sekondari Kwaluguru.
Mbunge wa Jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vyumba vya maabara vya sekondari ya Kwaluguru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Kweinjugo kata ya Kwaluguru wilaya ya Handeni
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza ngoma ya asili ya wazigua .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika ambapo aliwaambia wajifunze kupima mambo ya viongozi wa siasa wasije wakaingizwa kwenye matatizo bila kutarajia kwani wapo zaidi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na si ya wananchi ndio maana wanadiriki kutangaza maandamano wakati wao wenyewe hawapo wameenda nje ya nchi kupumzika.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakazi wa Handeni kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Handeni ambapo aliwaambia watu wanatakiwa kupewa fursa na kurahisishiwa maisha yao hivyo kodi ndogo zinatakiwa ziangaliwe upya kwani zimekuwa kero kwa wafanyabiashara ndogo ndogo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na madereva wa boda boda wa Chanika Handeni.
Watu wakiwa wamemzunguka Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kumaliza mkutano wake Soko la zamani Chanika wilayani Handeni.
No comments:
Post a Comment