Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Bima la Taifa (NIC) katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa jijini Arushaa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid, ,aliyeshika mice ni meneja wa shirika hilo Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin Ole KambaineMeneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin Ole Kambaine akitoa maelezo mafupi kuhusu shirika hilo kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa mara baada ya kutembelea banda hilo jijini Arusha katikati ni meneja masoko na utafiti wa shirika hilo kutoka makao makuu Bw.Elisante MalekoMdau aliyetembelea banda hilo la Shirika la Bima la Taifa (NIC) akiwa anauliza maswali yanayohusu shirikika hilo lengo nikutaka kufahamu zaidi shughuli za shirika, kushoto ni Afisa wa Bima Bi.Costancia KomanyaMeneja masoko na utafiti wa shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoka makao makuu Bw.Elisante Maleko akiwa anatoa ufafanuzi kwa mdau aliyefika katika banda lao ambapo alisema kuwa pamoja na bima nyingine pia wanatoa huduma ya bima ya matibabu (madecare) ambao ni mpango maalum wa shirika hilo kutoa matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kaumwa na michango ni midogoMuonekano wa banda la shirika la Bima la Taifa (NIC) katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabaranijijini Arusha
Meneja masoko na utafiti wa shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elisante Maleko amewataka watanzania kuona shirika hilo ni mali yao kwa kuwa shirika hilo ni mali ya umma na michango ni midogo hivyo kila mwananchi kumudu
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliyotembelea banda lao katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid jijini Arusha
Bw.Maleko alisema kuwa shirika hilo lina bima ya matibabu amabayo ni mpango maalum wa shirika hilo kutoa kinga ya matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kuumwa na michango ni midogo na kila mwananchi anamudu kujiunga na huduma zinapatikana nchi nzima
Pia alisema Bima za nyumba inakinga na majanga ya wizi,moto,tetemeko na mafuriko hivyo kuwataka wananchi kukatia nyumba zao bima.
No comments:
Post a Comment