Monday, September 22, 2014

Shirika la nyumba latoa mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vijana mkoani Pwani


 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Pwani Pauline Mrango akisoma Hotuba ya makabidhiano ya mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa Pwani.
Shirika la Nyumba la Taifa limetoa mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 12 pamoja na mafunzo kwa vijana ya wiki mbili ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa shilingi laki tano kwa kila kikundi kama mtaji .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani.

Mgeni rasmi aliyepokea mashine hizo ni Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa kwenye ziara  mkoani Pwani.

Baada ya kupokea mashine hizo, Mgeni rasmi alijibu risala ya meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Pwani  kwa  kutoa shukrani kwa  Shirika la Nyumba, kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na Shirika la Nyumba hususani katika uendelezaji wa makazi pamoja na kusaidia vijana  kujijengea uwezo wa kujiajiri. Pia alilisifia Shirika la Nyumba kwa kutoa msaada wa mashine hizi katika hamlamsahuri zote nchini.

Mgeni rasmi alisisitiza kauli ya Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete ya kuziagiza Halmashauri za miji na Wilaya kuipatia NHC Ardhi bure, kwa kuziagiza Halmashauri za Mkoa wa Pwani kuipatia NHC ardhi  kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba hasa za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu ununuzi wa nyumba hizo.

Pia aligusia suala la serikali kuondoa kodi ya thamani (VAT) katika mauzo ya nyumba za NHC ili kuliwezesha Shirika kujenga na kuuza  nyumba  bora  kwa gharama nafuu kwa manufaa ya watanzania wote.


No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...