Monday, September 22, 2014

ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE JIMBO LA BAGAMOYO

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua maktaba ya shule ya msingi ya Jitegemee iliyopo kata ya Magomeni mjini Bagamoyo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, Kinana yupo katika ziara ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa akiongozana na Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. PICHA NA KIKOSIKAZI  CHA FULLSHANGWE-BAGAMOYO) 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Bagamoyo  Dk. Shukuru Kawambwa akielekeza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Magomeni mjini Bagamoyo, Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi.4Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza akizungumza jambo na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwinshehe Mlao.5Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwinshehe Mlao akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Jitegemee kata ya Magomeni mjini Bagamoyo.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya msingi Jitegemee kata ya Magomeni Bagamoyo8Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.9Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Bagamoyo  Dr. Shukuru Kawambwaakiwahutubia wapiga kura wake hawapo pichani.11Baadhi ya wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama wa CCM leo mjini Bagamoyo.12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Pwani wakila kiapo cha utii kwa chama cha Mapinduzi kutoka kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Joyce Masunga,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwinshehe Mlao na kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmde Kipozi.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Bagamoyo  Dr. Shukuru Kawambwa13Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akitema cheche katika mkkutano huo.

No comments:

MATUMIZI YA BARUTI YAONGEZEKA NCHINI

  MATUMIZI ya Baruti nchini yameongezeka kutoka wastani wa tani 3,000 kwa mwaka katika miaka ya 1990 hadi kufikia wastani wa tani 26,516.0...