Thursday, September 25, 2014

AIRTEL YATOA VITABU KWA SHULE YA SEKONDARI SHIBULA MWANZA

DSC05496[1]Meneja Airtel Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (Kushoto) na Afisa
  Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Juma Kasandiko
  wakiwa wameshikilia kitabu baada ya  makabidhiano ya vitabu vya shule
  ya Sekondari Shibula vyenye thamani ya shilingi millioni moja na nusu
  vilivyotolewa na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu.
DSC05493[1]Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Juma
  Kasandiko (kulia)  akimkabithi vitabu  mkuu wa shule ya shule ya
  Sekondari Shibula James Chisanda vilivyotolewa na Airtel chini ya
  mpango wake wa Airtel Shule yetu,
DSC05501[1]
DSC05502[1]Waalimu wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu mara
baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airte kukabithi vitabu hivyo
chini ya mpango wake wa  Airtel shule yetu ambapo shule hiyo imepokea
  vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja
  na Laki tano
DSC05505[1]Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu vya
  sayansi walivyokabidhiwa na Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel,
chini ya mpango wa Airtel  shule yetu Airtel ilikabithi vitabuvya
sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na nusu kwa shule
hiyo
DSC05418[1]
DSC05419[1]Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakiwa katika picha ya pamoja
wakati wa halfa ya kupokea msaada wa vitabu kutoka kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel
Press Release
  Airtel yatoa vitabu kwa shule ya sekondari Shibula Mwanza
  Mwanza, Jumanne 23 Septemba 2014, Wanafunzi wa shule ya sekondari
Shibula iliyoko Mkoani Mwanza wamefaidika na vitabu kupitia mradi wa
  Airtel shule yetu  ambapo Airtel imetoa msaaada wa vitabu vya sayansi
  vyenye thamani ya shilingi milioni moja na Laki tano
  vitakavyowawezesha wanafunzi hao  kupata elimu bora.
  Kwa zaidi ya miaka 10 sasa mpango huu wa Airtel shule yetu umekuwa
ukisaidia  shule za sekondari kwa kuwapatia nyenzo muhimu kma vile
vitabu, vifaa za kufundishia , madawati, kuboresha majengo ya shule
  lengo likiwa ni kuboresha ubora katika kutoa  elimu nchini.
  Akiongea wakati wa hafla ya kikuabithi vitabu Meneja Mauzo wa Airtel
kanda ya Ziwa Bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel imewekeza kiasi cha
  kutosha katika kusaidia malengo mkakatika katika sekta ya elimu kwa
  kushirikiana na serikali katika kutoa elimu bora. Kwa kupitia mradi wa
  Airtel Shule yetu tumeweza kuzifikia shule zaidi ya 1000 zilizoko
  katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia vifaa vya kujisomea na
kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu huku tukifanikiwa  kupunguza
  uwiano wa kitabu kwa mtoto kutoka  watoto 6 kwa kitabu kimoja hadi
  watoto 2 kwa  kitabu kimoja.
Leo tunatoa vitabu vya  masomo ya sayansi ikiwemo Hisabati Fizikia,
  Kemia na Baiologia kwa shule ya Shibula sekondari tukiamini utachangia
  katika kuongeza kiasi cha ufaulu na kuchochea wanafunzi wengi kujiunga
  na masomo ya sayansi. Tutaendelea na jitihada hizi katika kuboresha
  sekta ya elimu na kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi nchini
  aliongeza Daudi.
  Kwa upande wake  Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemema Mkoani
Mwanza Juma Kasandiko ameishukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa
  shule za sekondari zilizoko mwanza na kuwaasa wanafunzi kutumia muda
  wao kujisomea na kuacha tabia ya utoro shuleni na kwa kufanya hivyo
  kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo na Mwanza kwa
  ujumla.
  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Shibula Bwana
  James Elias Chitanda alisema” Napenda kuwashukuru Airtel kwa kutoletea
  msaada huu wa vitabu shule ni hapa, vitabu ni nyenzo muhimu katika
  kuongeza maarifa na ujuzi hivyo vitabu hivi vitasaidia kuhamasisha
  wanafunzi wengi kujisomea  na  kuongeza upeo, vitawasadia walimu
  kuandaa masomo yao na kuwahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo
  ya sayansi na kuongeza idadi ya wanasayansi  kwa ujumla.Tunatoa wito
  kwa makampuni mengine kujiunga na kuchangia katika sekta ya elimu
  kwani ina mahitaji na changamoto nyingi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...