Shirika la nyumba la taifa(NHC) limetoa onyo kwa wapangaji wake wenye tabia ya kupanga na wakishapanga kwenye shirika hilo kuwapangisha wapangaji wengine waache mara moja tabia hiyo kwani kinyume na mkataba walioingia na shirika hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa shirika hilo mkoani hapa James Kisarika wakati akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake baada ya shirika hilo kugundua uvunjifu wa mkataba uliofanywa na mteja wao.
Kisarika alisema kuwa shirika hilo liliingia mkataba na mteja Mohamed Abdallah Dada kama ilivyo kawaida ya shirika hilo lakini wakati mktaba wa mteja huyo ulipoisha waligundua mteja aliekuwa kwenye nyumba 002 kitalu E kwenye barabara ya Sokoine si Yule walioingia nae mktaba hapo awali.
Alisema baada ya kugundua hivyo walifuata taratibu hizo kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Arusha na ndipo waligundua mpangaji aliepo siyo alieyepangisha kwani nae alikwisha mpangisha mteja wake WINNER STATIONARY ambapo mkataba wa mteja wa kwanza ulikuwa unakwisha July Mwaka huu.
“Hata hivyo shirika hiloi limemtoa mpangaji huyo kwa kukiuka mkataba wa shirika na shirika hilo litaandaa taratibu za kisheria dhidi ya mteja huyo zinaandaliwa na hiyo itakuwa fundisho kwa wapangaji wenye tabia kama hiyo”alisema kisarika.
Mapangaji wa shirika hilo Mohamed Abdallah Dada hakupatikana kuzungumzia hatma yake na shirika la nyumba kuhusu kadhia hiyo ya ukiukwaji wa mkataba wake na shirika la nyumba la taifa NHC.
Vyombo vya habari vilishudia maofisha wa Majembe waliofika dukani hap majira ya saa nne Asubuhi na kuanza kukata kufuli la duka hilo na kasha kuingia ndani kama amri ya shirika hilo iliyomtaka mteja huyo kuhakikisha anaondoa vitu vivyomo kwenye duka hilo ndani ya siku saba.
Nae mpangaji huyo wakiohojiwa na wanahabari waliokuwa wakishuhudia tukio hilo lililotekelezwa na kampuni ya Majembe Actionen Mart kwa niaba ya shirika hilo zoezi lililoenda vizuri bila ya vurugu yoyote Winner Stationary alisema kuwa hana la kusema kwa msemaji wao hayupo kwa sasa.
No comments:
Post a Comment