Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi na wafuasi wake 16 wa wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahari Kidavashari alisema kuwa viongozi hao walikamatwa Septemba 25,majira ya saa 11.30 asubuhi mtaa wa majengo mkabala na nyumba ya kulala wageni ya Dubai Kata ya Kashaulili Wilayani Mpanda.
Viongozi hao na waafuasi wao walikamatwa baada ya kufanya Maandamano bila kibali kwa ajili ya kuunga mkono maagizo yaliyotolewa na Viongozi wao wa Kitaifa ya kufanya maandamano nchi nzima kwa lengo la kuishinikiza Serikali isitishe Kikao Maalumu cha Bunge la Katiba na kusitishwa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Wanaoshikiliwa na Polisi ni Almasi Ibrahim Ntije Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Katavi, Abrahma Mapunda (16),Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda,Hamisa Kolongo (60) Katibu wa Chadema Mpanda.
Wengine waliokamatwa ni Lameck Constantino (37) Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mpanda na Mkazi wa Itenka, Mlokozi Bagasheki (30) Mwenyekiti wa Vijana Cretus Aloyce (320Katibu wa Jimbo la Mpanda na Shabani Ibrahimu (26)Katibu wa Vijana Chadema na mkazi wa Kotazi.
Mbali ya viongozi hao pia wafuasi wengine waliokamatwa ni Kenedy Zakayo (20) mwanachama mkazi wa kijiji cha Ilebula,Mariam Omary (43)Katibu muenezi wa Chadema, mkazi wa majengo,Fransisco Misigalo (29) mwenyekiti wa vijana Mkoa Mkazi wa Kashaulili,Selemani Hamisi (25) mkulima wa misunkumilo.
Wengine waliokatwa ni Anselemu Kanyengele (45) mkazi wa Majengo, Kasena Maulid Mjumbe wa Chadema Wilaya,Mwailwa James (35) mwanachama na mkazi wa kotazi, Emil Kalomo(30) mkulima,na Seif Ibrahimu(34) mwanachama na mkazi wa Majengo.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa viongozi wa chama hicho walieleza kuwa awali Chama hicho kiliandika barua hapo Septemba 22 kwa jeshi la polisi wakiomba kufanya maandamano tarehe 25 pamoja na Mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mpanda Hoteli
Hata hivyo barua hiyo ilijibiwa na jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda hapo Septemba 24 ikikitaka Chama kisifanye Maandamano wala Mkutano wa hadhara.
Kwa mujibu wa Maelezo ya Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda Idd Faraja alieleza kuwa Chama kiliamua kufanya maandamano hayo baada ya kufanya maandalizi ya maandamano hayo na jeshi la polisi kuchelewa kuwapatia barua ya kuwazuia kufanya maandamano na mkutano.
Akaeleza kuwa kitendo cha Jeshi laPolisi kuchelewa kujibu barua yao ya kuomba kibali walivyoona imekuwa kimya walijijua kuwa wamekubaliwa.wakaamua kufanya maamuzi ya kuandamana bila kibali.
Katika Hatua nyingine Ofisi za Chadema ambazo zipo katika Mtaa wa Majengo A’ jana kutwa nzima zilishinda zimezungukwa na Askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa na silaha chini, PIA Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Mpanda kiliimalishwa kwa Ulinzi baada ya kuwepo ulinzi kuhofiwa kuvamiwa na wafuasi wa Chadema walioonekana kuwa na hasira.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahari Kdavashari amewatahadharisha wananchi na wakazi wa Mkoa huo wa Katavi kutojihusisha na maandamano ya namna yeyote ya Kisiasa hadi hapo yatakaporuhusiwa.
Pia amewaasa kutoshawishiwa na chama chochote kushiriki maandamano au migomo kwani watakuwa wamekiuka sheria na taratibu za nchi.
No comments:
Post a Comment