Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akikabidhiwa zawadi ya fulana na Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo yenye ujumbe wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. katikati ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kulia ni kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika
Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga kulia akimpima uwezo wa kuona macho dereva wa kampuni ya usafirishaji wa abirianya Abood basi Morogoro, Augustino Mpepwa wakati wa uzinduzi wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya uzindui wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha.
DK YOHANA KIBONA KUMPIMA DC ANTHONY MTAKA AFYA KULIA NI DK CHARLES MSENGA MGANGA WA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU
DR YOHANA KIBENA akiwaandikisha madereva tayari kupimwa afya zao katika Hospitali ya Polisi ya Morogoro. TBL imefadhili upimaji wa afya hizo.
No comments:
Post a Comment