Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba wakati alipowasili katika kata ya Mbuzii ambapo ameshiriki katika ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM katika kata hiyo na kuzungumza na wananchi waliojitokeza kumpokea, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi mkoa wa Tanga akihimiza na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukiiarisha chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM, Kero kubwa katika mkutano huo ilikuwa ni kufungwa kwa kiwanda cha Chai cha Mponde ambacho wananchi wanataka warudishiwe ili wakiendeshe wenyewe ,Baada ya mwekezaji Yusuf Mulla kukiuka makubaliano ya kisheria jambo lililopelekea mmoja wa viongozi katika kata hiyo ambaye ni diwani Diwani wa Kata ya Guga Bw. Richard Mbunguni kufukuzwa mkutanoni na wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa madai ya kuwasaliti katika sakata hilo, Akizungumza na wananchi katika kutano huo Kinana ameahidi kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu akisema “Katika hili kila mtu aliyehusika abebe mzigo wake kwa kuwajibika” , ameahidi kurudi Mponde baada ya mwezi mmoja ili kuwapatia majibu sahihi wananchi yatakayomaliza kabisa mgogoro huo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BUMBULI -LUSHOTO)Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba alipokuwa akizungumza na jambo wakati alipowasili katika kata ya Mbuzii.Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba akizungumza na wanapiga kura wake wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaalipowasili katika kata ya Mbuzii.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Mbuzii wakati akiwa katika ziara ya kikazi katikajimbo la Bumbuli, Kulia anayeangalia ni Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa kikundi cha Bodaboda cha Dule B wakati alipozindua tawi lao na kukabidhi pikipiki iliyotolewa kwa kikundi hicho na mbunge wa jimbo hilo Mh. Januari Makamba katikaki pichani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi fungua za pikipiki kwa kiongozi wa kikundi cha Dule B Bw.Nuru ambayo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanakikundi cha Maisha Plus wakati alipotembelea kikundi hicho.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuponda kokoto wakati alipotembelea kikundi cha Maisha Plus ambacho hii ni moja ya kazi zinazofanywa na kikundi hicho.Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi akishiriki kazi ya kufyatua matofari huku mbunge wa jimbo hilo Mh. Januari Makamba akishuhudia wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokitembelea kikundi cha wajasiriamali cha Maisha Plus.Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi akiendelea na kazi ya kufyatua matofaliKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila muwa na Mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha ITV Ufoo Sari wakati alipotembelea kikundi cha wajasiriamali cha Maisha Plus jimboni Bumbuli leo miwa hiyo inazalishwa na kikundi hicho.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiranda mbao huku Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akishuhudiaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameshiriki pia kuchoma tanuri la matofari kwa kuwasha moto katika moja ya matundu ya tanuri hilo anayeangalia ni Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba .Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akizungumza jambo na mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari MakambaNape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mponde.Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini na Mchumi wa mkoa wa Tanga CCM akiwasalimia wananchi kwenye mkutatano wa hadhara uliofanyika kata ya Mponde jimbo la Bumbuli.Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo.Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo.Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo.Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mponde.Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akizungumza na wapiga kura wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mponde jimboni Bumbuli.Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM akimtoa katika eneo la mkutano huku akiwa amemshika mkono diwani wa Kata ya Guga Bumbuli Bw. Richard Mbuguni kulia aliyefukuzwa na wananchi katika mkutano huo wa hadhara kwa madai ya kuwasaliti na kushirikiana na mwekezaji .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment