Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Asha-Rose Migiro, akimpongeza Kada wa CCM, Asha Abdallah Juma, baada ya kumtunuku shahada ya pili ya Biashara, katika mahafali ya 25 ya chuo hicho, yaliyofanyika, Oktoba 26, 2013, Makao Makuu ya OUT, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Kushoto ni Makamnu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette. Asha ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC CCM, amewahi kuwa Waziri katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia Katibu wa NEC, Oganaizesheni.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Makao Makuu, Daniel Chongolo, akipongezana na Mjumbe wa NEC ya CCM, Asha Abdallah Juma baada ya wote kutuniwa shahada zao katika mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), yaliyofanyika Oktoba 26, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Chongolo ametunukiwa shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma na Asha shahada ya Pili ya Biashara. Katikati ni Kada wa CCM, Rachel Kyala ambaye pia ametunukiwa shahada ya Mawasiliano ya umma.Picha na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment