Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ukianzia Shule ya Kambangwa Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Meneja wa Samsung Tanzania Kishor Kumar, wapili ni Mkuu wa kitengo cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom, Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Bi.Theresia Ng’wigulu.
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akimfuatilia mwanafunzi Frank Massay wa shule ya sekondari ya Kambangwa akitumia komputa zilizounganishwa na Mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung. Pamoja nao katika picha (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule, Mkuu wa shule hiyo Bi.Theresia Ng’wigulu, na Mtaalamu wa komputa wa Samsung, Julius Giabe.
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame, akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari nchini na Mkongo wa taifa wa mawasiliano, uliofanyika kwa kuanzia na shule ya Msingi Kambangwa ya jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kambangwa, wakitoa burudani kwa wageni waalikwa, Wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari na Mkongo na Taifa wa Mawasiliano.
---
.Shule za Sekondari nchini kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
· Kupata komputa na vifaa vya umeme wa jua
Dar es Salaam, Oktoba 22 2013Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amezindua mpango wa kuziunganisha shule za sekondari nchini na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano huku akitanabaisha kuwa serikali inathamini na kutambua mchango wa sekta binafsi katika kuleta maendeleo kwa jamii inayo wazunguka.
Waziri Mbarawa amesema bila ya kuwa na sekta Rasmi ambayo inatambua mchango wake kwa jamii inayowazunguka upatikanaji wa maendeleo kwa jamii ya Watanzania ungeendelea kuwa mgumu, akitolea mfano mradi huo, Mradi ulioanzishwa na Vodacom na Samsung katika kuunga mkono mpango wa serikali wa kuunganisha shule za sekondari na mkongo wa taifa wa mawasiliano.
“Kama wewe ni mwekezaji au mmiliki wa kampuni binafsi na hautambui matatizo ya watu wanaokuzunguka sio jambo jema, Ni muhimu sehemu ya faida unayoipata uwekeze katika kutatua changamoto zinazowakabili, Tukijenga utamaduni huu tutaweza kuiokoa jamii ya kitanzania ambayo inahitaji misaada ya aina mbalimbali katika kujiendeleza” alisema Prof. Mbarawa.
“Kama ilivyo katika sekta ya Elimu Serikali pekee haiwezi kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta hii, bali tu ni kwa kushirikiana na wadau kama ilivyofanyika kwa Vodacom na Samsung kuwezesha mradi wa kuunganisha shule zetu na mkongo wa taifa wa mawasiliano.
Aidha Waziri Mbalawa alisema Serikali inunga Mkono harakati za kampuni hizo katika kuisaidia sekta ya elimu kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
“Dunia sasa imepita katika mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia bila kujenga uwezo na miundombinu katika shule zetu, kwa kutoa vifaa vya kuwawezesha wanafunzi wetu kujifunza kutokana na mabadiliko yaliyopo bado elimu yetu haitopiga hatua na jamii ya Watanzania itaendelea kuwa nyuma siku zite, Serikali inatambua mchango huu na inaahidi kuwaunga mkono wote ambao wana nia ya dhati ya kuleta mapinduzi katika elimu.”
Akitoa hotuba yake kwa Waziri Mbarawa, Mkuu wa kitengo cha Mfuko wa Huduma za jamii, Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule alibainisha kwamba jitihada hizi zinakwenda sambamba na malengo ya kutoa huduma za kimawasiliano pamoja na kuunga mkono juhudi za watanzania katika kufikia malengo ya Mpango wa maendeleo ya Millennia (MDGs).
“Elimu ndio ufunguo wa maendeleo ya jamii yoyote ile; kwa sababu hiyo Vodacom inafanya kila jitihada kuhakikisha wanafunzi wanapata nyenzo bora za kujifunzia bila ugumu wa aina yoyote ile. Pia katika jamii yoyote ile duniani yapaswa kuzingatia maendeleo ya kitekinolojia yanayojitokeza, tumekuja kuhakikisha tunawezesha shule zote nchini zinakuwa na uwezo wa kuyafikia maendeleo hayo.” Alisema Mwakifulefule na kuongeza.
“Kampuni yetu imejidhatiti katika kuendelea kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu, Hivi punde tumeanzisha mpango wa kuziwezesha shule zilizoko maeneo ya karibu na minara ya Vodacom inayotumia nishati ya jua kuzalisha umeme kupata nishati ya hiyo.” Alisema.
Mwakifulefule alihitimisha kwa kusema Vodacom Foundation, imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kujenga madarasa na kuyawezesha kwa vifaa mbalimbali, pia imeziwezesha shule hizo kwa kuzipatia vifaa mbalimbali vya kujifunzia nchi nzima.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania, Dongha Jang kampuni yake ina dhamira ya dhati ya kuleta mapinduzi ya elimu kupitia mradi huu ambao pia unatumia Jenereta ya umeme jua, (Solar) ambayo itakua ikitoa nishati kwa vifaa vitakavyo kuwa vinatumika.
“Kwa kuimarisha nishati ya jua, tunaweza kuzihudumia jamii za kiafrika na nishati ambayo inapatikana kwa bei rahisi mno, ambayo pia ni rafiki wa mazingira hivyo kwa kuanzia na shule ya kambangwa na shule nyingine zitakazo fuata zitanufaika na mradi huu.” Alisema Jang.
“Samsung imeamua kuelekeza nguvu zake katika kutatua matatizo ya kielimu lengo kuu ni kuunga mkono kuendeleza jitihada za viongozi wa Afrika na pia kupata nguvu kazi iliyoelemika ambayo ndiyo msingi mkuu wa waajiriwa wa baadae.” Aliongeza Jang.
Kampuni imehamisha nguvu zake kutoka jitihada za kuwajibika na shughuli mbalimbali za kijamii na kuunda kitu ambacho kitathaminiwa na jamii kwa pamoja. Hii ina maana kwamba, shughuli zote za kielimu, kiafya pamoja na mipango ya kuendeleza jamii itakuwa na madhumi mawili; ya kuunga mkono kufikia malengo ya kibiashara ya kampuni na vilevile kuboresha maisha ya waafrika kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment