Mkuu wa Idara ya
Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda, akiongea
na waandishi wa Habari(hawapo pichani)wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani
ya Shilingi Milioni kumi na mbili, itakayotumika kwa ajili ya mkutano mkuu wa
mwaka wa wahariri wa vyombo vya habari utakaofanyika Iringa hivi karibuni, wanaoshuhudia
kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom
Tanzania (Vodacom Foundation) Bw.Yessaya Mwakifulefule na Mwenyekiti wa jukwaa
la wahariri nchini Bw. Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa jukwaa
la wahariri nchini, Bw.Absalom Kibanda (kushoto)akikabidhiwa hundi yenye
thamani ya Shilingi Milioni kumi na mbili na Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma
na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Joseline Kamuhanda, kwa ajili ya mkutano
mkuu wa mwaka wa vyombo vya habari utakaofanyika Iringa hivi karibuni
Anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa jukwaa hilo Bw. Neville Meena.
No comments:
Post a Comment