Friday, October 25, 2013

MAANDALIZI YA JUKWAA LA SERENGETI FIESTA 2013 KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB

 
Jukwaa la kisasa kabisa na ambalo halijawahi kutumika katika tamasha lolote kubwa ambalo limewahi kufanyika nchini hapa likionekana katika taswila tayari kwa maandalizi kamili ya Serengeti Fiesta 2013 inayotarajiwa kuunguruma hapo kesho kuanzia majira ya saa 12 jioni ndani ya Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pichani ni sehemu ya maandalizi ya jukwaa la kisasa litakalotumika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar.

Jukwaaa hilo linatarajiwa kujumuisha makamuzi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya zaidi ya 50 huku wasanii  kutoka nje ya nchi watadodoka zaidi ya 4 na ratiba ya mwaka huu itakuwa ya aina yake kwani wasanii wanatarajiwa kuanza kutumbuiza mapema zaidi ya siku zingine zote.

Serengeti Fiesta ya mwaka huu imeonyesha uzalendo kuanzia katika viingilio vya kushuhudia makamuzi ya wasanii wa nje na ndani ya nchi,kwani burudani zote zitapatikana kwa kiasi cha shilingi elfu 10 kwenye vituo vya kuuzia na shilingi 15 kwa watakao nunulia mlangoni.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...