Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole (kushoto) akipokelewa na Msaidizi wa Rais katika masuala ya jamii Mwanahamisi Kitogo (kulia) kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada ya kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ( kulia) akisalimiana na Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole (kushoto) kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwonesha tisheti yenye nembo ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel mara baada kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimvalisha tisheti yenye nembo ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole ikiwa ni ishara ya kumteua kuwa balozi wa WAMA, alipoitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa uboreshaji afya – WAMA Dk. Sarah Maongezi .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwonesha khanga iliyobuniwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel yenye maandishi ya ‘mtoto wa mwenzio ni mwanao mkinge na ukimwi’ kwenye ofisi za mara baada kuitembelea ofisi hiyo jana jioni jijini Dares Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimuonyesha Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole kinyago kinachoonyesha umoja wa watanzania wakati balozi huo alipozitembelea ofisi za WAMA hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo kwa Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole, kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea jana jioni jijini Dares Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ( kulia) akizungumza na mama mzazi wa Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole, Partricia Oduwole (kushoto) kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini jijini Dares Salaam. Aliyebebwa ni Ismachiah mdogo wake na Zuriel.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ( kushoto ) akiwa na Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole, kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam.Picha na Magreth Kinabo – Maelezo
----
Na Magreth Kinabo-MAELEZO
MKE wa Rais Mama Salma Kikwete , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) amemtunuku Balozi wa kuwatetea watoto wa kike katika masuala ya elimu kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole kuwa mwanachama (balozi) wa heshima wa taasisi hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mama Kikwete mara baada ya Zuriel kuitembelea ofisi ya WAMA iliyoko Ikulu jijini Dares Salaam na kufanya mazungumzo kuhusu shughuli inazozifanya .
Mama Kikwete alimwezea Zuriel jinsi taasisi yake inavyofanya kazi mbalimbali ikiwemo ya kuhakikisha watoto wa kike yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi wanapata elimu ili waweze kuajiriwa na kujiajiri ikiwa ni hatua ya kuendeleza maisha yao ya baade na kutimiza ndoto zao.
Kwa mujibu wa baba wa Zuriel, Ademola Oduwole alisema mtoto wake pia amekuwa akihamasisha wasichana kubadili mtazamo wa Bara la Afrika kwa kuwa huko Marekani watu hawalijuwi bara hilo na wanadhani ni bara la njaa .
“Amezindua mradi wa dreaming up dreaming big’ lengo lake ni kuwahamasisha watoto wa kike kuwa na ndoto za kuendelea,” alisema Oduwole.
Oduwole aliongeza kuwa Zuriel anapenda kuhamasisha kuhusu suala la elimu kwa kuwa ndio njia ya kufikia malengo ya milinea.
Alisema Zuriel ameshatembelea nchi Nigeria,Malawi na Tanzania ambapo alifika Shule ya Msingi ya Olympio na Shule ya Sekondari ya Jangwani na Shule ya Sekondari ya wasichana ya Marian.Pia ameshafanya mahojiano na marais wanane wa Afrika , ambao ni wa Tanzania, Mauritius, Kenya,Nigeria, Cape Verde,Sudan ya Kusini na Liberia.
Kwa upande wake Mama Kikwete alifurahishwa na juhudi za Zuriel na kumtaka kuendelea kufanya mambo makubwa katika kutimiza ndoto zake.
Naye Zuriel alishukuru kwa ukarimu alioupata kwa Watanzania na ameaihidi kuitangaza Tanzania na WAMA mahali popote duniani.
Zuriel alikuwepo nchini kwa kipindi cha siku sita kuanzia jumapili iliyopita akiwa na wazazi wake na wadogo zake Azaliah Arielle na Ismachiah, amerejea Marekani mwishoni mwa wiki hii.
No comments:
Post a Comment