Wednesday, October 23, 2013

Katiba kicheko Vyama Vyote Vyama vya Upinzani



 Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula(Kushoto)akifurahia Jambo na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa  baada ya kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam jana
Viongozi wa vyama vya siasa,(kushoto)Isaack Cheyo(UDP), Nancy Mrikaria(TLP), Fahmi Nassoro Dovutwa (UPDP), James Mbatia NCCR-Mageuzi, Profesa Ibrahim Lipumba(CUF), Philip Mangula(CCM) na Dk Willibrod Slaa(Chadema)wakiwa wameshikana mikono baada ya kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix 
---
Serikali inatarajia kuandaa hati ya dharura ili kuwezesha kufanyika kwa maboresho ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba ambayo yatajadiliwa upya katika Mkutano wa Bunge unaoanza Oktoba 29 mjini Dodoma.

Tayari vyama vya upinzani na chama tawala vimekubaliana taratibu muhimu za kufuata ili maboresho hayo yaweze kupita ndani ya Bunge. Muswada huo haukuwa umepangwa kujadiliwa katika mkutano ujao wa Bunge ndio maana itabidi iombwe hati hiyo ya dharura. Hatua hiyo ni ushindi kwa vyama vitatu vya upinzani vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi, ambavyo vilipinga muswada huo wakati wa mkutano uliopita wa Bunge Septemba, mwaka huu.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea..............

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...