Mbunge wa Iramba-Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba.
---
Watanzania nchini Uingereza wamejitayarisha kuhudhuria mkutano wa wazi siku ya Jumamosi mchana ili kumsikiliza Mbunge wa Iramba Magharibi Ndugu Mwigulu Nchemba. Huu ni mwendelezo wa ziara alizofanya Ndugu Nchemba na ujumbe wake akitokea Marekani alipopokewa na mamia ya watanzania na makada wa CCM nchini huko.
Aidha katika ziara zake nje ya nchi ndugu Nchemba ameweka bayana msimamo wa CCM na Serikali yake katika hatua za makusudi za kuhakikisha watanzania nje ya nchi wanatambulika katika mipango madhubuti ya kitaifa na kwamba wakati umefika wa rasilimali za wanadiaspora kuanza kutumika kujenga nchi yao bila uwoga.
Uchunguzi wetu umefanya mawasiliano na kubaini kuwa watanzania toka majiji mbalimbali ya hapa Uingereza watasafiri kuhudhuria mkutano huo ili kujua serikali imeandaa mbinu gani mpya za kutatua kero za watanzania wanaoishi diaspora. Mkutano huo ambao utaambana na meza ya vyakula na vinywaji itakayoandikwa na mpishi maarufu wa kitanzania na baadaye kufuatiwa na muziki utafanyika katika ukumbi maarufu na wa kisasa wa St. Patrick's 100, Beaumont. Leys Lane.
Leicester. LE4 2BD.
Na Leyla Shomari,
Tanzania Now: Freelance Observers: Slough. St.Marys Road. SL3
Na Leyla Shomari,
Tanzania Now: Freelance Observers: Slough. St.Marys Road. SL3
No comments:
Post a Comment