Meneja wa Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Gloria Minja akizungumza jambo wakati wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili waweze kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu , chakula na malazi leo jijini Dares Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Tabu Likoko akifungua majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili waweze kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu , chakula na malazi leo jijini Dares Salaam.Kushoto ni mjumbe wa majadiliano hayo kutoka WAMA ,Julius Jacob
Mjumbe wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe wa kuwatambua na kuwahudumia watoto waishio katika mazingira hatarishi , Asha Mtwangi akichambua ujumbe wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’ inayosimamiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dares Salaam.
Mjumbe wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe wa kuwatambua na kuwahudumia watoto waishio katika mazingira hatarishi, Peter Mabwe akichambua ujumbe wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’ inayosimamiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dares Salaam.
|
Mjumbe wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe wa kuwatambua na kuwahudumia watoto waishio katika mazingira hatarishi , Asha Mtwangi akichambua ujumbe wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’ inayosimamiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dares Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya ushauri katika mitaala, uandishi na uhariri , Victor Msinde (katikati )akichangia mada juu ya majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili waweze kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu , chakula na malazi leo jijini Dares Salaam.Picha zote Eleuteri Mangi –MAELEZO.---
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SEKTA binafsi na taasisi mbalimbali zimeshauriwa kufadhili katika kuwasaidia watoto wanaoshi katika mazingira magumu badala ya kusaidaia matamasha pekee ikiwa ni hatua mojawapo ya ya kuwapatia maisha bora , ikiwemo kupunguza umasikini na tatizo hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Gloria Minja wakati wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili waweze kusaidia watoto hao.
“Tuzinaomba sekta binafsi ikiwa ni moja wa wadau katika kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu katika malengo yao walijiwekea kupitia kipengele cha Uwajibikaji katika jamii (yaani corporate social responsibilities) kubadili mtanzamo wa kusaidia matamasha pekee ,bali waanze kufanya hivyo kwa watoto hawa ili nao waweze kusoma ,kutibiwa na kupata malazi,” alisema Gloria.
Alisema ikiwa sekta hizo zitatekeleza wajibu huo,watoto hao wataweza kupata fursa ya kusoma , kupata kazi na kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ili waweze kuendesha maisha yao.
Gloria aliongeza kuwa mbali sekta hiyo , Serikali na kila mwanajamii wanawajibu kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao , kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwawezesha kupata mahitaji muhimu na kupunguza tatizo la umaskini nchini.
Akizungumzia kuhusu ujumbe uliokuwa unatengenezwa na wadau hao kutoka sekta binafsi na Serikali alisema lengo lake litakuwa ni kutoa ushawishi kwa jamii nzima ili iweze kuwatambua na kuwahudumia watoto hao.
Aidha alisema ujumbe huo utatumika kuhamasisha katika kampeni ya utetezi kwa watoto hao ili Serikali, Jamii na sekta binafsi zitambue kuwa jukumu la kuwalea watoto hao ni la pande zote.
Akifungua majadiliano hayo Kaimu Katibu Mtendaji wa WAMA , Tabu Likoko alisema kuwa taasisi hiyo inafanya kazi ya kusaidia elimu kwa watoto wa kike, yatima na uwezeshaji kwa wanawake.
Mradi huo wa Pamoja Tuwalee unatekelezwa katika mikoa ya Morogoro,Pwani, Dares Salaam na Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu,ambapo ulianza kutekelezwa mwaka 2011 hadi mwaka 2013 na WAMA kwa ushirikiano wa fhi360 chini ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani(USAID).
No comments:
Post a Comment