Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete mwishoni mwa juma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa shati lililotengenezwa na wanafunzio wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete baada ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa juma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongeana wananchi wa kijiji cha Ivalalila wilayani Makete baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha afya cha kijiji hicho mwishonimwa juma.
Rais akitoka kuweka jiwe la msingi madarasa ya kidato cha tano shule ya sekondari lupalilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Bi Sarah Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji pamoja na mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili October 28, 2009 baada ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha Lupalilo wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akihojiwa katika TV na kueleza kuwa maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake wote kuteketea kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga akimshukur Rais kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha yake kwani sasa anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo.Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment