Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile, Kamishna wa Sera Bw. Beda Shallanda na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa majadiliano ya mkutano wa madola.
Mwenyekiti wa majadiliano ya mkutano wa Madola Bw. Sheku Sesay akifafanua jambo.
Picha juu na chini ni Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano; mwenye tai nyekundu ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile.Picha zote na Bi. Eva Valerian – Washington DC
---
Wakati mikutano mingine ikiendelea hapa mjini Washington DC, Tanzania pia inashiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Madola ambao utafanyika kwa siku mbili mfululizo. Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe wote ambao ni nchi wanachama.
Katika mkutano huo kikubwa kilichojadiliwa ni kuhusiana na suala zima la biashara, ni namna gani biashara inaweza kufanyika na kwamba nchi zetu haziko vizuri sana katika uwanja huu wa kimataifa. Katika mkutano huo walijadili ni jinsi gani wanaweza kufanikisha lengo la kuanzisha mfuko ambao utatumika kusaidia biashara ‘trade facilitation’.
Katika majadiliano yaliyokuwa yakifanyika wajumbe wengi walipenda kujua kwamba ni tofauti gani mfuko huo mpya utaleta ili nchi zetu ziweze kunufaika. Hiki ni kitu kikubwa zaidi kilicho wagusa wajumbe wengi.
Akizungumza na vyombo vya habari Dkt. Silvacius Likwelile ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye alisema kuwa”katika mkutano huu jambo ambalo limezungumziwa sana ni kuhusu kuondoa vikwazo ambavyo mara nyingi tunawekewa ili kufikia masoko katika ulimwengu”.
Aliendelea kusema kuwa, ni imani yetu kwamba tume ya madola itafanyia kazi masuala hayo ili hatimaye tuwe na msimamo mmoja wa kuweza kusaidia ukuaji wa biashara katika nchi zetu.
Mkutano huu utaendelea tena kesho na inategemewa utakuwa na mafanikio makubwa.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha Washington D.C
No comments:
Post a Comment