Waandishi wa habari wakifuatilia kwa kina mkutano huo jini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu katika mahojiano na ITVMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu katika mahojiano na ITV
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusu kampeni hiyo ya mauzo
Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Kyando Mchechu amezindua kampeni ya uuzaji wa
nyumba za gharama nafuu ambao umebebwa na kauli mbiu iitwayo “NYUMBA YAKO,
MAISHA YAKO”.
Kupitia kampeni hii, Mkurugenzi Mkuu alisema Shirika limezindua
rasmi programu ya ujenzi wa nyumba 5,000 (elfu tano). Kampeni imezinduliwa Oktoba tatu mwaka huu.
Alifafanua kuwa kampeni ni
ya muda mrefu na imelenga uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za gharama nafuu.
Alisema kuwa katika awamu ya kwanza Shirika limeanza na nyumba (2,000) elfu mbili
ambazo zimefikia katika hatua tofauti ya ujenzi.
Maeneo yaliyoanza kunufaika na
mpango huu ni pamoja na Mvomero (Morogoro), Mkinga (Tanga), Lindi, Mkuzo
(Ruvuma), Bombambili (Geita), Mlole (Kigoma), Ilembo (Katavi), Kongwa (Dodoma),
Unyankumi (Singida), Kibada ( Dar Es Salaam) na Mrara (Babati).
Uzinduzi
huu umekuwa wa aina yake kwa kuwa kabla ya Mkurugenzi Mkuu kuzungumza na Wanahabari,
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Biashara Bw. David Shambwe alifanya semina fupi na
Wanahabari ili kufafanua juhudi zinazofanywa na Shirika katika ujenzi wa miradi ya gharama nafuu na pia changamoto
mbalimbali zilizopo katika ujenzi huo.
Bw. Shambwe alichukua nafasi hii
kuwafahamisha Wanahabari kuwa mauzo ya nyumba hizo yataanza rasmi tarehe 13
Oktoba 2013. Lengo ni kuwaandaa wanunuzi ili itakapofika tarehe 13 Oktoba wawe
wamejiandaa kununua nyumba hizo. Shirika litaufahamisha
umma wa Tanzania kupitia vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment