Ujumbe wa Tanzania katika majadiliano, kutoka kushoto
ni Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda,
Kamishna Idara ya Sera Bw. Beda Shallanda, Mkurugenzi
wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe
na Bw. Said Magonya Kamishna wa Fedha za Nje akielezea jambo.
Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Yusuph Mzee kulia,
akisoma kwa makini taarifa zitakazowasiliswa katika
mikutano hiyo mbele ya ujumbe kutoka Tanzania.
Toka shoto ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa,
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata
Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius
Likwelile, Mkurugenzi wa Idara ya kupunguza Umasikini
MKUKUTA Bi. Anna Mwasha pamoja na Kamishna Mkuu
wa TRA Bw. Harry Kitilya wakisikiliza kwa makini.
Ujumbe wa Tanzania wakisikiliza kwa makini hoja
zinazotolewa na Waziri wa Fedha hayupo pichani
ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho.
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya
Mipango Dr. Philip Mpango, Naibu Gavana wa BOT Bi.
Natu Mwamba na Mchumi wa Benki Kuu Bi. Sauda Msemo
wakisikiliza kwa makini.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa (kushoto),
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata
Mulamula wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akiwa katika
majadiliano na ujumbe wa Tanzania kuhusu maandalizi ya
mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Kutoka kushoto ni Kamishna wa Idara ya Sera Bw. Beda
Shallanda akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utafiti na
Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe.
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata
Mulamula akimsikiliza kwa makini Afisa Mwambata
anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji
ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw.
Paul Mwafongo
Picha zote na Bi. Eva Valerian – Washington DC
No comments:
Post a Comment