Tuesday, October 08, 2013

NBC YAZINDUA MWEZI WA HUDUMA KWA WATEJA

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe (kulia) na Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye (kushoto) wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi rasmi wa promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya NBC ikiwa ni moja ya matukio yatakatokwenda sambamba na maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.  Zawadi zote katika promosheni hiyo zitagharimu zaidi ya shs milioni 300.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Andrew Massawe (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya NBC ikiwa ni moja ya matukio yatakatokwenda sambamba na maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Zawadi kubwa ni gari jipya aina ya Suzuki Swift toleo la mwaka 2013. Katikati ni  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale na kushoto ni Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale (katikati), akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe na Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye.
  Meneja katika kitengo  cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa cha NBC, Dorothea Mabonye (kushoto) akitoa ufafanuzi jinsi ya uendeshaji wa promosheni ya Weka Upewe wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...