Friday, October 04, 2013

Baraza La Madiwani lamtupia Lawama Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi

 MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akitoa risala ya kufungua kikao cha Baraza la Madiwani kilicho kutana jana katika Ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaam Jana.  

Pamoja na mambo Mengine Meya Silaa amemtupia lawama Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga  kuwa ndio chanzo cha kusimamishwa kazi kwa  aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Gabriel Fuime kwa kuandika barua ya malalamiko dhidi yake na Waziri Mkuu kuuagiza uchunguzi kufanyika huku mkurugenzi huyo akiondolewa kazini. 

Silaa akiongelea suala hilo huku akipigiwa makofi na madiwani alisema analaani vikali migogoro ya kisiasa isiyo na tija kwa wananchi ambao ndio wapiga kura. 
  Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa akipitia nyaraka mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa katika mkutano huo.
Baadhi ya madiwani wakiwa ndani ya kikao hicho.
Mbunge pekee kutoka Manipaa ya Ilala ambaye amesifiwa kwa kuhudhuria vikao hivyo vya Baraza la Madiwani Ilala, Mussa Zungu akiwa katika Baraza hilo jana

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...