(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
……………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wamefanya ziara ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Ziara ya wajumbe hao wa kamati Ufundi ilianza kwa kukagua kazi ya ukarabati wa kituo yalipo matangi ya maji eneo la Chuo Kiukuu cha Dar es salaam, maungio ya mradi wa bomba jipya yaliyopo eneo la Mpiji, ujenzi wa ofisi ya mradi wa bomba kuu la maji kutoka Ruvu Juu zilizopo Kibaha, kukagua mabomba yaliyohifadhiwa eneo la Kibaha Mwendapole na upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu Mladizi na Ruvu darajani.
Akifanya majumuisho ya ziara hiyo Mwenyekiti wa wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya DAWASA Christine Kilindu amesema kuwa wajumbe wameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miundo mbimu hiyo ambapo matarajio mradi huo utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa mwishoni mwa mwaka huu.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani watarajie kupata huduma ya maji iliyo bora mara miradi ya Ruvu Juu Chini itakapokamilika.
Aidha, Christine amewaasa wananchi wa maeneo yanapopita mabomba wa miradi hiyo kuyatunza vizuri kuanzia wakati huu yalipohifadhiwa na yatakapokuwa yameanza kutumika ili yawanufaishe wananchi wote wa mikoa hiyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi DAWASA Romanus Mwang’ingo alisema kuwa pamoja na kuboresha huduma kwa maeneo yaliyo pembezoni mwa barabara ya Morogoro yaani Kimara, Mbezi, Kiluvya, Kibaha, Visiga, Mlandizi na Kibamba, utekelezaji huo pia utawanufaisha wakazi wa Ubungo, Vingunguti, Kimara, Tabata na Kinyerezi ambao nao wanahudumiwa na mtambo unaotoa maji kutoka Ruvu Juu.
Mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini unalenga kuongeza uzalishaji maji na kuwahudumia wakazi wa maeneo ya uwekezaji (EPZ), Chasimba, Buma, Zinga, Kerege, Mpiji, Bunju, Wazo, Salasala, Madale, Kinzudi, Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala.
Kazi hiyo ya maboresho inafanyika chini ya mpango maalumu wa kuboresha huduma ya upatikanaji wa Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es salaam na maeneo mengine yanayohudumiwa na DAWASA unaohususha ujenzi wa miradi mipya na pamoja na kukarabati miundombinu iliyopo.

No comments:
Post a Comment