Tuesday, January 27, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI CHARLES MWIJAGE WAANZA KAZI RASMI KWA KUTEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI

1
Mtaalamu kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro iliyopewa kazi ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I Clas-Eirik Strand (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) Katikati ni Meneja Mradi wa Kinyerezi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima.
2
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage akisalimiana na baadhi ya wataalamu kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro iliyopewa kazi ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I mara baada ya kuwasili kituoni hapo. Aliyeambatana naye kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
3
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi.
4
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio kwenye eneo la mradi wa Kinyerezi I.
5
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye eneo la kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I.
6
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima ( aliyetangulia mbele) akiongoza msafara wa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene kwenye eneo la mradi.
7
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (katikati) akielezea maendeleo ya mradi wa Kinyerezi I. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene. Kushoto kabisa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
10
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akifafanua jambo katika ziara hiyo.
13
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuchakata gesi cha Kinyerezi.
17
Sehemu ya mtambo wa kuchakata gesi wa Kinyerezi
18
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage.
16
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na wataalamu wa mradi wa kuchakata gesi wa Kinyerezi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...