Monday, January 26, 2015

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIK AZINDUA TAWI JIPYA LA UCHUMI SUPERMARKET MBEZI KAWE

001
Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi SuperMarket (Afrika mashariki), Jonathan Ciano (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik katika ufunguzi wa Tawi jipya la Uchumi lililoko Mbezi Kawe karibu na ukumbi wa Rainbow jijini Dar es Salaam.
002
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Said Meck Sadick akizungumza na wasambazaji na Wafanyakazi wa Uchumi Supermarket wakati wa Uzinduzi wa Tawi Jipya la Duka hilo.
003
Mbunge wa Nyamagana Mwanza Ezekiel Wenje, katikati akichagua moja ya Tiketi katika Shindano la kumtafuta mshindi wa shindano lijulikanalo kama ” Mimi Mwana Hisa “ kulia ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha Emanuel Ndaki , na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi Supermarket (Afrika mashariki), Bw. Jonathan Ciano
004
Mbunge wa Nyamagana Mwanza, Ezekiel Wenje katikati akinyosha juu moja ya Tiketi katika Shindano la kumtafuta mshindi wa shindano lijulikanalo kama ” Mimi Mwana Hisa “ kulia ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Emanuel Ndaki na kushoto ni mkurugenzi wa Uchumi Supermarket,(Afrika mashariki) Jonathan Ciano na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick, ambapo Elizabeth Robert ameibuka Mshindi wa Shindano hilo.
005
Mkaguzi mwandamizi toka bodi ya Michezo ya kubahatisha Emmanuel Ndaki (kulia) akionyesha Namba ya Mshindi wa “Mimi Mwanahisa” katikati ni Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje na kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Uchumi Supermarket (Afrika mashariki) Jonathan Ciano, katika shindano lililoendeshwa na Uchumi Supermarket na kuchezeshwa katika Tawi jipya la Uchumi lililoko Mbezi Kawe karibu na ukumbi wa Rainbow-Mbezi chini jijini Dar es Salaam,ambapo Elizabeth Robert mkazi wa jiji la Dar es salaam amejishindia zawadi ya hisa zenye thamani ya milioni tano za kitanzania.
006
Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi Supermarket,(Afrika mashariki) Bw.Jonathan Ciano (kushoto) akiweka Saini kwenye mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh Milioni Tano, baada ya mkazi wa kinondoni kujishindia kiasi hicho katika Shindano lililoendeshwa na kampuni hiyo.
007
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick katikati akikata Utepe kama ishara ya Uzinduzi wa tawi Jipya la Uchumi Supermarket lililoko Mbezi Kawe karibu na ukumbi wa rainbow-mbezi chini jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Uchumi SuperMarket (Afrika mashariki) Bw.Jonathan Ciano na Kulia ni Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje.
008
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik na Mkurugenzi mkuu wa Uchumi Supermarket(Afrika mashariki) Bw. Jonathan Ciano na Meneja wa Uchumi Supermark tawi la Mbezi Kawe, Bw. Evans Munga wakikata keki baada ya Uzinduzi wa tawi jipya

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...