Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mh Egon Kochanke akitoa historia fupi ya wahanga wa maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi katika maadhimisho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Utamaduni wa Russia na kuandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania.
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi Usia Nkhoma akiwakaribisha wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar ambavyo Kuna Klabu za Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa utamaduni wa Russia wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na kuwakumbuka wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi.
Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akimwelezea Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati alipotembelea katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia ambapo baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu waliweza ushiriki katika Kuadhimisha na Kuwakumbuka Wahanga Wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi
Balozi wa Ujerumani, Mh Egon Kochanke akisoma moja ya bango lililobandikwa katika Ukumbi wa Utamaduni wa Kirusi wakati wa Maadhimisho ya Wahanga wa Mahangamizi Makuu ya moto yanayofanyika kila tarehe 27 January kwaajili ya kumbukumbu
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Kibasila, Azania na Kisutu wakisoma moja ya bango lenye historia fupi ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto.
Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akimwelezea Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati alipotembelea katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia ambapo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo waliweza kupata historia fupi ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto
Wanafunzi wakifuatilia historia fupi ya Wahanga iliyokuwa ikitolewa na Afisa Habari wa UN, Bi Usia Nkhoma
Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akitoa neno mbele ya Mgeni rasmi ambae ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya maadhimisho na kumbukumbu ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi ambapo maadhimisho hayo ufanyika kila tarehe 27 Januari.
Picha Zote na Josephat Lukaza -Lukaza Blog<
No comments:
Post a Comment